Tetesi za Usajili Ligi Kuu NBC Tanzania Bara
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026 unakaribia kuanza, na tayari vilabu vikubwa nchini vimeshaanza kusuka vikosi vyao kwa kufanya usajili wa wachezaji na makocha wapya. Katika makala hii, tunakuletea muhtasari wa tetesi na taarifa rasmi za usajili kwa klabu za Simba SC, Young Africans SC (Yanga), Azam FC, na Singida Big Stars.
Simba SC Yathibitisha Usajili wa Wachezaji Sita na Kumbakiza Kocha
Simba Sports Club imeanza usajili wake kwa kishindo baada ya kuthibitisha kuwasaini wachezaji wapya sita pamoja na kumwongezea mkataba kocha wao mkuu.
- Jonathan Sowah – Straika mwenye uwezo mkubwa wa kuchana nyavu
- Hussein Daudi Semfuko – Kiungo chipukizi mwenye kasi na nguvu
- Morice Abraham – Beki wa kati mwenye umbo na uzoefu mkubwa
- Allasane Maodo Kanté – Kiungo mshambuliaji raia wa Mali
- Mohammed Omar Bajaber – Mchezaji wa kimataifa wa Zanzibar
- Kocha Fadlu Davids – Amedumu Simba na ataendelea kuwaongoza kwa msimu ujao
Yanga SC Yasajili Kikosi Kipya Chenye Makali ya Afrika
Young Africans SC, mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania, wameingia sokoni kwa nguvu na kusajili mastaa kadhaa pamoja na kocha mpya.
- Kocha Mkuu Romain Folz – Kocha wa Kifaransa anayepewa nafasi kubwa Afrika
- Lassine Kouma – Beki kutoka Afrika Magharibi
- Mousa Balla Konté – Kiungo mchezeshaji
- Andy Boyeli – Straika wa Kongo, anayetajwa kuwa mwarobaini wa safu ya ushambuliaji
- Ecua Celestin – Kiungo mwenye uwezo wa ku-control game kwa ufanisi
- Abubakar Ninju – Winga machachari kutoka Zanzibar
- Abdulnassir Mohammed ‘Casemiro’ – Kiungo wa ulinzi mwenye nguvu na umakini
- Offen Chikola – Beki wa kulia anayesifika kwa overlapping
Azam FC Yamtangaza Florent Ibengé Kuinoa Azam FC
Klabu ya Azam FC imemteua rasmi Florent Ibengé kuwa kocha mkuu mpya kwa msimu wa 2025/2026, akitarajiwa kuleta mabadiliko ya kiufundi na kurejesha ubabe wa Azam katika mbio za ubingwa. maarufu kama Florent Ibengé, ni kocha na mchezaji wa zamani wa soka mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Amezaliwa mnamo Desemba 4, 1961, na anajulikana sana kwa mafanikio yake katika kusimamia vilabu mbalimbali barani Afrika pamoja na timu ya taifa ya DRC. Ibengé alijipatia heshima kubwa alipokuwa kocha wa AS Vita Club na baadaye kuiongoza timu ya taifa ya DRC kufikia hatua ya nusu fainali ya AFCON mwaka 2015 na kutwaa nafasi ya tatu. Pia amewahi kufundisha vilabu vya Ulaya, ikiwemo Ufaransa na Uchina
Singida Big Stars Yafanya Mapinduzi kwa Kumsajili Kocha Miguel Ángel Gamondi
Katika harakati za kupambana na timu kubwa msimu ujao, Singida Big Stars wametangaza rasmi usajili wa Miguel Ángel Gamondi kutoka Argentina,lakini alishawahi kuwa kocha mkuu wa Young Africans ambaye ana historia ya kufundisha vilabu vikubwa Afrika Kaskazini.


- Soma Pia
- Jonathan Sowah Asema Yupo Tayari Kuchana Nyavu za Wapinzani
- Yanga Wamemsajili Ecua Celestin – Mshambuliaji Hatari
- Young Africans SC wamemsajili Andy Boyeli – Mshambuliaji Mpya wa Magoli
- Allasane Maodo Kanté – Mchezaji Mahiri kutoka Senegal
Ligi Kuu Tanzania Bara NBC Premier league.
Hitimisho
Dirisha la usajili 2025/2026 linaonekana kuchukua sura ya kiushindani zaidi huku vilabu vikijaribu kujiimarisha kwa ajili ya mashindano ya ndani na kimataifa. Tunaendelea kufuatilia tetesi na usajili rasmi wa wachezaji, makocha, na mipango ya vikosi kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara.
Tembelea Wikihii Michezo kwa taarifa za hivi punde kuhusu usajili, mechi, matokeo na ligi kuu Tanzania.