Katili ndani ya uwanja halafu Mwanamitindo nje ya uwanja
Mpira wa miguu na fashion vimekua vikienda pamoja miaka mingi sana kama unamkumbuka David Beckham na Fashion styles zake miaka hiyo, Hivi sasa mchezaji MLINZI wa Barcelona na Ufaransa, Jules Koundé amekua kivutio cha wengi baada ya kuwa ni mchezaji lakini pia ni mwanamitindo njue ya uwanja
MLINZI wa Barcelona na Ufaransa, Jules Koundé, amecheza mechi 100 mfululizo kwa timu zote mbili, kuanzia Novemba 28, 2023 alipoanza dhidi ya Porto katika Ligi ya Mabingwa. Tangu wakati huo, amekuwa akiichezea Barcelona na Ufaransa kila mara, akiwa kama mchezaji anayeanza au kutoka benchi.
–
Katika msimu huu pekee, Koundé amecheza mechi 55, ambapo 47 ni kwa Barcelona na 8 kwa Ufaransa.
–
Baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Real Betis, mlinzi huyu anatarajiwa kuanza tena kwenye mechi ijayo dhidi ya Dortmund, huku akikaribia kuvunja rekodi ya klabu ya Antonio Torres ya mechi 136 mfululizo.
–
Hadi sasa, Koundé amekamilisha mechi 82 mfululizo kwa Barcelona na 18 kwa Ufaransa.
Ni mchezaji haswa beki kisiki lakini upande wa pili ni bonge la blazamen (bishoo) wa kwenda anapiga pamba hatari na ni official mwanamitindo wa kampuni yake anayoimiliki.



