Kylian Mbappé atimiza ndoto yake Bernabéu
BAADA ya kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kujiunga na Real Madrid, Kylian Mbappé ameweka wazi kuwa uamuzi huo ulikuwa rahisi mno kwake. Katika mahojiano na La Sexta, mshambuliaji huyo wa Kifaransa amesema furaha yake ya kuvaa jezi ya Real Madrid na kucheza katika dimba la Santiago Bernabéu ni kitu alichokitamani tangu utotoni.

–
“Kuchagua kati ya Real Madrid au pesa haikuwa uamuzi mgumu,” amesema Kylian Mbappé.
–
“Nilitaka tu kucheza Santiago Bernabéu nikiwa nimevaa jezi ya Real Madrid. Nilichotaka ni kuwa mwenye furaha… Real Madrid ni furaha kwangu, ndoto yangu kubwa tangu nikiwa mtoto.”
–
“Siwezi kuifikiria Real Madrid bila Vinicius Jr! Nimejiunga na Madrid nikiwa na wazo wazi la kucheza sambamba na Vinicius pale Bernabéu,” Mbappé aliambia La Sexta.

–
#spotileo #spotileoupdates #michezo #mbappe #vinijr #realmadrid