Mamelodi Sundowns wamepigiwa makofi na mashabiki wa Esperance Sportive de Tunis
Mamelodi Sundowns imeendelea kuwa gumzo ugenini kwa wenyeji kukubali uwezo wao, Mashabiki wa Esperance Sportive de Tunis wamewapongeza Sundowns baada ya dakika tisini.
Baada ya kuwarushia Makopo wachezaji wao (Esperance Sportive de Tunis) sasa ikawa zamu ya Mamelodi Sundowns kurudi vyumbani ndipo mashabiki wa Esperance wakasimama kwa pamoja na kuanza kuwapigia makofi huku wakiimba jina la Peter Shalulile na Ronwen Williams.
Mamelodi Sundowns imewahi pigiwa makofi na mashabiki wa Wydad Casablanca na Al Ahly Sporting Club ugenini.

Kwa kifupi mashabiki wa soka kule Kaskazini wanavutiwa na soka la @sundownsfc.
#sundowns
#mamelodisundowns #esperance #TotalEnergiesCAFCL