Stephane Aziz Ki ni mchezaji mshambuliaji na ni muhimili pale Yanga SC, akiwa na nafasi kubwa katika mafanikio ya klabu. Kumbakisha Stephane Aziz Ki ni jambo zuri sana kwa Yanga kutokana na ubora aliouonesha Azizi Ki tangu alipotua Yanga na hata hivyo timu nyingi za Africs zimekuwa zikimmendea Azizi Ki kwa karibu sana.
Katika msimu uliopita, Aziz Ki alifunga mabao 21 kwenye Ligi Kuu NBC na kupiga pasi za mwisho 8, na kuiwezesha Yanga kutwaa ubingwa huku yeye akiibuka mfungaji bora. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, alihusika na mabao manne katika mechi 12, akifunga mabao mawili na kupiga pasi mbili za mwisho, na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya robo fainali.

Ofa zilizopo mezani kutoka kwa timu mbalimbali, historia ya kuamua matokeo ya mechi kubwa, pamoja na ushawishi mkubwa alionao kwa vigogo wa timu hiyo, ni mambo ambayo yameishawishi Yanga kuhakikisha wanambakisha mchezaji huyo raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 28.
Timu nyingi ndani na nje ya bara la Afrika, zikiwemo Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns, na Orlando Pirates, zimeonesha nia ya kumsajili mchezaji huyu. Kwa mashabiki wa Yanga, kumbakisha Stephane Aziz Ki ni ishara ya uhakika kwamba klabu itaendelea kuwa na nguvu katika ligi na mashindano mbalimbali.
Stephane Aziz Ki ataendelea kubaki Yanga baada ya kukubaliana na klabu kuongeza mkataba ambao unasemekana utamfanya kua ni moja kati ya wachezaji wanaolipwa pesa ndefu Tanzania.
Mkataba mpya wa Aziz Ki Yanga Ni kwa makubaliano ya pande mbili yaani Aziz Ki na Yanga na kwamba atakuwa analipwa mshahara unaokadiriwa kufikia dola 13,000 (sawa na shilingi milioni 35) kwa mwezi kwa msimu wa 2024/2025.