Mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez Awasha Moto
MSHAMBULIAJI wa Inter Milan, Lautaro Martenez ameendeleza moto aliokuwa nao msimu uliopita.
–
Msimu uliopita alifunga mabao 35 na kutoa assist nane lakini alibeba mataji matatu, alikuwa mfungaji bora wa Serie A,MVP Serie A na mfungaji bora Copa America lakini hakupewa nafasi kwenye Tuzo za Ballon d’or .
–
Msimu huu ni kama amerejea tena akitaka heshima aliyonyimwa msimu uliopita.
–
Jana alifunga bao moja kwenye ushindi wa Inter wa mabao 2-1 dhidi ya Bayern Munich kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufikisha mabao saba kwenye ligi ya mabingwa msimu huu.
–
Martenez amekuwa mchezaji wa kwanza wa Inter Milan kufikisha mabao saba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu Samuel Eto’o alipofanya hivyo.

–
#Spotileo #Spotileoupdates ##Michezo #michezoonlineupdates #Football #champions #Championsleague #Inter Milan #lautaro