Ratiba NBC Premier League 2025/26 Yatangazwa Rasmi
Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imetangaza ratiba kamili ya NBC Premier League 2025/26 ikiwa na matukio makubwa yanayovutia mashabiki mapema kabisa: mzunguko wa ufunguzi unaanza Septemba 17–18, 2025, kisha dirisha la mechi za kimataifa za FIFA na raundi za CAF limepangwa katikati ya kalenda ili kulinda ushindani wa ndani.
Dabi ya Kariakoo ndiyo kipengere kinachoteka vichwa vya habari: Yanga vs Simba itapigwa Desemba 13, 2025 kwenye Benjamin Mkapa, kisha Simba vs Yanga Aprili 4, 2026 (ROUND 22) kwa marudiano—vipindi viwili vinavyoweza kuamua kasi ya mbio za ubingwa msimu huu.
Kalenda pia imepangwa kwa uangalifu kuakisi windows za kimataifa na michuano ya klabu Afrika (CAF), hivyo klabu zitahitaji usimamizi bora wa squad, mbinu za mzunguko (rotation) na saikolojia ya mechi kubwa, hasa wiki zinazoambatana na viporo.
- Tazama ratiba kamili ya mechi: Ratiba ya Ligi Kuu (Wikihii)
- Chanzo rasmi TPLB: Ratiba ya NBC 2025/26
- Msimamo “live” wa NBC: Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
- Updates za haraka: Jiunge na WhatsApp Channel ya Wikihii Sports
Kwa mashabiki na wadau, hizi ni tarehe za kuweka kwenye kalenda: mwanzo wa ligi (Sept 17–18), Dabi ya kwanza (Dec 13), na marudiano (Apr 4). Taarifa nyingine—ikiwemo viporo, mabadiliko ya muda/uwanja au ratiba za CAF/FIFA—zitaendelea kusasishwa kwenye kurasa tajwa hapo juu