Simba SC vs Al Masry SC | Kinawaka kwa mkapa stadium leo 9/4/2025
Leo ndio Leo Mnyama Simba anataka kulipa kisasi kwa mgeni wake Al Masry SC katika uwanja wa mkapa stadium jijini Dar es salaam Tanzania, Simba wakiwa kamili wamewaahidi mashabiki zao kwamba wanaenda kupindua meza dhidi ya Al Masry SC,
Simba SC inacheza nyumbani dhidi ya Al Masry SC kwenye Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa Leo Jumatano, Apr 9, 2025, 13:00 UTC. Hii ni Robo Fainali (1/4) ya Hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF, Mchezo huu utarushwa Live bila chenga kupitia kituo chako bora kwa matangazo ya mpira Africa AZAM TV
Simba alipoteza mechi ya kwanza kwa jumla ya mabao 2 – 0 hivyo leo ndio siku ya mnyama kulipa deni kwa waarabu Al Masry SC

Hakikisha umelipia Kisimbuzi chako kama ni cha antena au dish au hata kama unatumia card fanya malipo mapema ili kuondokana na usumbufu utakaoweza kujitokeza, hautakiwi kupitwa na hii mechi ni mechi ya mwisho kwa SIMBA SC Itakayoamua hatima ya SIMBA Kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Lakini pia ubora wa simba kupindua matokeo kwenye uwanja wa mkapa unaifanya hii mechi kuwa ngumu sana kwa pande zote mbili.
Mnyama simba kupitia wanahabari wake wamesema wapenzi wa simba wafike kwa wingi uwanjani kwani mnyama anaenda kupindua matokeo mchana kweupe,

Simba SC vs Al Masry SC | Kwenye Odds
Rekodi ya sasa ya timu hizo ni Simba SC kushinda 0, Al Masry SC kushinda 1, na sare 0. Simba SC wana odd 1.50 kushinda, 3.60 kwa sare, na 6.50 kwa Al Masry SC kushinda. Simba SC ndio wanapigiwa upatu kushinda mechi hiyo, kwa mujibu wa waweka kamari.
