Wachezaji Wanaolipwa Mshahara Mkubwa Tanzania
Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea kuwa Bora Africa na sasa imefikia viwango vya juu ikiwa namba nne 4 kwa ubora Africa, maana yake NBC Premier league imepanda thamani kubwa kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika mchezo huu tanzania, kitu ambacho kimefanya wachezaji mbalimbali kujipatia mishahara mikubwa kutokana na vipaji vyao vya kucheza soka.
Wachezaji wa mpira wa miguu wenye vipaji nchini Tanzania wameweza kupata fursa za kucheza katika vilabu vikubwa (Simba, Yanga, Azam, Singida BS) na kupata malipo makubwa kutokana na juhudi wanazoweka uwanjani
kumekuwa na ongezeko kubwa la mishahara kwa wachezaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa thamani ya ligi za ndani na ushirikiano wa vilabu vya Tanzania na wadhamini wakubwa. Kwenye hii article tunaenda kuangalia wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa tanzania na sababu za wao kulipwa kiasi kikubwa kwenye timu zao.
Stephane Aziz Ki
Stephane Aziz Ki anakadiliwa kupokea kiasi zaidi ya Tsh 30,000,000. Ki ni mchezaji muhimu katika kikosi chake, akijulikana kwa uwezo wake wa kucheza kama kiungo mwenye nguvu na mbunifu uwanjani. Ufanisi wake umeweza kuvutia vilabu vikubwa na kumfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi nchini.
Clatous Chama
Clatous Chama anakadiliwa kupokea kiasi cha Tsh 28,000,000. Chama ni mchezaji wa kimataifa mwenye umahiri wa hali ya juu, hasa katika nafasi ya kiungo mshambuliaji. Uwezo wake wa kutengeneza nafasi na kufunga mabao umemfanya kuwa na thamani kubwa kwa klabu yake na kumuwezesha kupata malipo makubwa.
Ali Ahamada
Ali Ahamada anakadiliwa kupokea kiasi cha Tsh 25,000,000. Ahamada ni mlinda mlango mwenye uzoefu mkubwa na ujuzi wa hali ya juu katika kulinda lango ambae kwa sasa anachezea klabu ya Azam Fc. Uwezo wake wa kuokoa mipira migumu na kutoa mwongozo kwa safu ya ulinzi umefanya kuwa mlinda mlango bora na mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri nchini Tanzania.
Feisal Salum
Feisal Salum anakadiliwa kupokea kiasi cha Tsh 23,000,000. Salum ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa akichezea nafasi ya kiungo ambaye amejijengea jina kutokana na uwezo wake wa kudhibiti mchezo na kupiga pasi za mwisho pamoja na kufunga magoli ya mbali. Kutokana na Umahiri wake na mchango wake alioonesha akiwa anachezea klabu ya Yanga Sc, Fei toto aliweza kuivutia Azam Fc ambayo ilitambua uwezo wake na kumpa moja kati ya mikataba minono na kujiingiza kwenye orodha rasmi ya wachezaji wanaolipwa pesa nyingi Tanzania 2024.