Facebook wameanzisha utaratibu wa malipo kuwalipa content creators watakaotimiza vigezo na masharti ya META kampuni mama ya facebook, Meta wanalipa kupitia Facebook Pages au Facebook Proffesional Account, kinachotakiwa ni kutimiza vigezo ambavyo vinatofautiana kwa Pages na Proffesional Mode.
Kila mtu anaweza kumiliki Facebook Page au Facebook Proffesional Account
Kwenye Facebook Page au Facebook Proffesional Account unaruhusiwa kuweka maudhui (videos) ya aina yeyote ile ilimradi yasipingane na sheria za kupost videos/picha/maneno facebook, facebook hawaruhusu maudhui ya ngono, mauaji, na mambo ya hatari ambayo facebook wameelezea HAPA
Kila mtu ana uwezo ktk jambo fulani ambalo anaweza kulizungumzia au kulifanya akiwa LIVE au Akijirekodi iwe ni kutoa ELIMU fulani, Maelekezo fulani, Utaratibu fulani, Historia fulani, au Jambo lolote lile liwe la Kuelimisha au Kufurahisha/Kuchekesha haijalishi ilimradi usivunje zile sheria za Facebook na za nchi pia.
Soma Hii: Jinsi ya kufungua youtube channel na utaratibu wa kulipwa
Kila mtu anaweza kufanya hii kitu kwa sababu kila mwanadamu kuna sekta anaifahamu na anaweza kumuelewesha mwingine aelewe pia, kama wewe ni msusi wa nywele, mfugaji wa kuku, mkulima, mpishi, muuza duka, fundi nyumba au nyingine yeyote ile fahamu kwamba hakuna kinachokuzuia kumiliki biashara ya facebook page au proffesional account na kuanza kupost contents.
Jinsi ya kufungua Facebook Proffesional Account
Proffesional account ni rahisi sana ki msingi kama tayari unayo account ya kawaida facebook basi unachotakiwa kufanya ki kwenda kwenye settings the tafuta sehemu iliyoandikwa TURN ON PROFFESIONAL MODE ukibofya hayo maneno utakuwa tayari umefanikiwa kujiunga kwenye FB-Proffesional Mode na ukishabofya hapo kama imekubali unatakiwa uanze kuona analytics za contents zako facebook
Jinsi ya kufungua Facebook Page
Kufungua facebook Page nenda kwenye account yako kushoto uki scroll kwenda chini angalia sehemu itakayokuwa imeandikwa PAGES, Utabonyeza hapo kisha zitatokea options kama vile Manage Pages na Create New Page, utabonyeza Create New Page na hapo utajaza informations kama majina ya page yako picha (profile, cover)
Jinsi ya kulipwa na facebook
Ili kuanza kulipwa utaratibu unatofautiana kdg kwa Page na Proffesional mode Kwa Pages unatakiwa kuwa na Followers kuanzia 10,000 na masaa ambayo watu wameangalia contents zako, wakati kwenye Facebook Proffesional Mode unatakiwa kuwa na Followers zaidi ya 1000 tu na masaa kadhaa ambayo unayapata kwenye videos zako