Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025: Form five selection
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kidato cha tano yametoka hii leo 2025, Wanafunzi na wazazi sasa wanaweza kuangalia form five selection kwa kufuata utaratibu ambao tunaenda kukuelekeza kwenye hili chapisho
TAMISEMI husimamia mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati kwa mwaka 2025. Lengo kuu ni kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu anapata nafasi stahiki ya kuendelea na masomo. Uchaguzi huu unahusisha wanafunzi kutoka shule za serikali, binafsi, na watahiniwa wa kujitegemea.
Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi hupangwa kwenye shule za vipaji maalum kama Kilakala, Mzumbe, Ilboru, na nyinginezo. Wengine hupelekwa katika shule za kawaida za bweni au kutwa, au katika vyuo vya kati na vya ufundi.
Mchakato huu huanza baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne, ambapo wanafunzi hufanya mabadiliko ya machaguo yao kupitia mfumo wa Selform. Kisha, upangaji wa wanafunzi hufanyika kulingana na ufaulu wao na nafasi zilizopo. Majina ya waliochaguliwa hutangazwa rasmi baada ya hatua zote kukamilika.
Iwapo na wewe ni miongoni mwa wanafunzi au wazazi wanaosubiri matokeo hayo ya Form Five Selection 2025, hapa chini tunakuletea taarifa muhimu kuhusu jinsi ya kuangalia majina au jina lako, vigezo vya upangaji, nyaraka za kuripoti shule, na nini cha kufanya kama hujachaguliwa.
Majina ya Selection za Form Five 2025 Yanatoka Lini?
Kwa kawaida, TAMISEMI hutangaza majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwishoni mwa mwezi Mei au mapema Juni. Hii hutegemea kukamilika kwa uchakataji wa nafasi na tathmini ya ufaulu wa kitaifa.
Kwa mwaka huu 2025, inatarajiwa kuwa majina yatakuwa hewani kati ya tarehe 25 Mei hadi 10 Juni 2025 kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI:
Vigezo Vilivyotumika Kupangiwa Shule
TAMISEMI hutumia mfumo wa kielektroniki kuhakikisha upangaji wa wanafunzi unazingatia haki, sifa, na matakwa ya mwanafunzi. Baadhi ya vigezo ni:
- Ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE 2024)
- Machaguo ya mwanafunzi (kombinations & shule alizopendekeza kupitia SELFORM)
- Idadi ya nafasi zilizopo katika shule husika
- Jinsia na mahitaji maalum (kwa shule maalum za wasichana/ wavulana au zenye mafunzo ya kipekee)
- Uwiano wa mikoa, kuhakikisha usawa wa kitaifa
Fomu za Maelezo ya Shule (Joining Instructions)
Baada ya majina kutangazwa, kila mwanafunzi aliyechaguliwa ataweza kupakua fomu ya maelezo ya shule (joining instructions) kupitia tovuti hiyo hiyo ya TAMISEMI.
Fomu hiyo itaeleza:
- Mahitaji ya mwanafunzi (mavazi, vifaa vya shule, michango)
- Tarehe rasmi ya kuripoti
- Maelekezo ya usafiri na mawasiliano ya shule
- Kanuni na taratibu za shule husika
Je, Ni Lini Matokeo ya Tamisemi Kidato cha Tano 2025 Yatatangazwa?
Kama ilivyoelezwa awali, matokeo ya TAMISEMI Form Five Selection 2025 yanatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa Mei au mapema Juni 2025. Wanafunzi wataweza kuyapata kwa:
- Kutembelea https://selform.tamisemi.go.tz
- Kuingiza namba ya mtihani au jina la mwanafunzi
- Kupakua joining instructions ya shule aliyopangiwa
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Form Five 2025 (Hatua kwa Hatua)
- Tembelea Tovuti ya TAMISEMI: Nenda moja kwa moja kwenye https://selform.tamisemi.go.tz.
- Bonyeza Linki ya “Form Five First Selection 2025”.
- Chagua Mkoa Uliosoma: Tafuta jina la mkoa wako kwenye orodha iliyopo.
- Chagua Halmashauri Yako: Baada ya mkoa, chagua halmashauri inayohusiana na shule yako.
- Chagua Shule: Tafuta shule uliyosoma ili kuona kama umechaguliwa.
- Angalia Majina: Majina ya wanafunzi waliochaguliwa yataonekana pamoja na shule au chuo walichopangiwa.
- Pakua Maelekezo ya Kujiunga: Ukiiona nafasi yako, fuata maelekezo ya kujiunga kwenye tovuti hiyo hiyo.
Nyaraka za Msingi Unazohitaji Kuripoti Shuleni
Unapopangiwa shule, unahitaji kuwa na nyaraka hizi muhimu unapokwenda kuripoti:
- Fomu ya maelezo ya shule (Joining Instruction) iliyochapishwa
- Cheti cha kuzaliwa (au nakala)
- Cheti cha matokeo ya kidato cha nne (CSEE 2024)
- Picha ndogo za pasipoti (passport size photos)
- Kitambulisho cha mzazi/mlezi (au barua kutoka serikali ya mtaa/kijiji)
- Nakala ya kadi ya NHIF (kama ipo) au uthibitisho wa bima ya afya
Je, Ikiwa Sitachaguliwa Katika Raundi ya Kwanza?
Usihofu! Kwa kawaida, TAMISEMI hutoa nafasi ya mzunguko wa pili (second selection) kwa wanafunzi ambao hawakupangiwa shule katika raundi ya kwanza.
Kwenye raundi hii, wanafunzi hupewa fursa nyingine ya kuchagua shule zenye nafasi zilizobaki, na uteuzi hufanywa kwa kuzingatia ufaulu wao na nafasi zilizopo.
👉 Ni muhimu kufuatilia taarifa rasmi kutoka TAMISEMI au kurasa zao za mitandao ya kijamii ili usipitwe na mchakato huo.
Hitimisho

Kupangwa shule ya sekondari ya kidato cha tano ni hatua ya kihistoria kwa kila mwanafunzi. Kwa mwaka huu 2025, TAMISEMI inaendelea na jitihada kuhakikisha mchakato huu unafanyika kwa haki, uwazi, na kwa wakati.
Wazazi na wanafunzi wanashauriwa kufuatilia kwa ukaribu taarifa kupitia tovuti ya TAMISEMI au kupitia vyombo vya habari vya kuaminika.
Wikihii itakuwa na updates zote muhimu — hakikisha unaturudia kwa habari mpya!