Katika mambo ambayo serikali kupitia TRA pamoja na Polisi wamelifanya kwa ustadi wa hali ya juu ni hili jambo linalokuwezesha kuangalia deni la gari mtandaoni – TMS Traffic Check. Hii ni huduma mpya na ya kisasa kupitia kifaa chako kama ni simu au Laptop unaweza kuangalia faini za gari lako barabarani tofauti na ilivyokuwa zamani.
Jinsi ya kuangalia deni la gari TMS Traffic Check
Kutokana na urahisi wa kuweza kuangalia taarifa hasa zinazohusu faini ya gari yako kwa uharaka na kwenye smartphone yako ni jambo linalochochea uwajibikaji kwa dereva ikiwa ni pamoja na kutambua makosa na faini zake, Hata madereva ambao hawana tabia ya kuwa na makosa makubwa wanaweza kukutana na faini bila kutarajia. Kuangalia deni la gari lako mara kwa mara kupitia TMS Traffic Check kuna manufaa yafuatayo:
- Epuka Usumbufu: Kujua mapema kuhusu faini zilizojificha kutakusaidia kuepuka matatizo makubwa baadaye.
- Hakikisha Unadhibiti Faini Zako: Hakikisha unalipa faini zako kwa wakati na epuka vikwazo vinavyoweza kujitokeza kwa kuchelewa kulipa.
- Fuatilia Malipo: Angalia kama malipo yako yamepokelewa na kurekodiwa vyema, kuhakikisha kila kitu kiko sawa.

Jinsi ya Kuangalia Deni la Gari (TMS Traffic Check)
Kufuata hatua hizi ni rahisi na itakupa matokeo kwa haraka:
- Pata Taarifa Muhimu:
- Hakikisha unayo namba ya usajili ya gari lako na namba ya kumbukumbu ya faini, ikiwa inapatikana.
- Tembelea Tovuti Rasmi ya TMS Traffic Check:
- Fungua kivinjari chako na uende kwenye tovuti ya TMS Traffic Check kwa kutafuta “TMS Tanzania Traffic Check” kwenye Google, au tembelea moja kwa moja: https://tms.tpf.go.tz.
- Ingiza Namba ya Usajili wa Gari
- Kwenye tovuti, utaona sehemu tatu za kuchagua
- Search by Registration – Hapa unatazama deni kwa kutumia namba ya usajili wa gari lako
- Search by License – Hapa unatazama deni kwa kutumia leseni ya udereva
- Search by Reference – Hapa unatzama deni kwa kutumia control number
- Bonyeza Alama ya “Tafuta”
- Baada ya kuingiza taarifa, bonyeza kitufe cha “Tafuta” ili kuona matokeo kuhusu faini zinazohusiana na gari lako.
- Pitia na Lipa (Kama Inahitajika)
- Mfumo utakuonyesha orodha ya faini zote, ikiwa zipo, na taarifa kuhusu kosa, kiasi cha faini, na tarehe ya mwisho ya kulipa. Ikiwa kuna faini ya kulipa, tovuti itakuongoza jinsi ya kulipa, iwe kwa mtandao, kupitia benki, au kwa kufika kituo maalum cha malipo.
Jinsi ya Kulipia Deni la Gari
Baada ya kujua kiasi cha faini yako, unaweza kulipa kwa njia mbalimbali:
- Kulipa Deni la Gari Kupitia Tovuti ya TMS
- Ikiwa unahitaji kulipa faini zako mtandaoni, TMS Traffic Check itakupa maelekezo ya malipo. Unaweza kufanya malipo kupitia mfumo wa benki au kwa kutumia huduma za malipo mtandaoni.
- Kulipia Deni la Gari Kupitia Simu za Mkono (Mobile Payment)
- M-Pesa:
- Piga *150*00#
- Chagua “Lipa kwa M-Pesa”
- Chagua “Malipo ya Kampuni”
- Chagua “King’amuzi” kisha “Azam TV” (sawa na malipo ya faini)
- Ingiza namba ya kumbukumbu ya faini
- Weka kiasi cha faini
- Ingiza PIN yako na uthibitishe malipo
- Airtel Money:
- Piga *150*60#
- Chagua “Lipa Bili”
- Chagua “Faini za Trafiki”
- Ingiza kiasi cha faini na namba ya kumbukumbu
- Weka PIN na uthibitishe
- Tigo Pesa / Mixx by Yas:
- Piga *150*01#
- Chagua “Lipa Bili”
- Chagua “Faini za Trafiki”
- Ingiza kiasi cha faini na namba ya kumbukumbu
- Weka PIN na uthibitishe
- M-Pesa:
- Kulipia Deni la Gari kwa Kutembelea Benki au Kituo cha Malipo
- Pia, unaweza kulipa kupitia benki zinazoshirikiana na TMS au kwa kutembelea vituo vya malipo vilivyoteuliwa na Mamlaka ya Usafiri nchini. Tafadhali hakikisha kuwa umekamilisha malipo na umepokea stakabadhi ili kuepuka matatizo yoyote ya kisheria baadaye.
Hitimisho
TMS Traffic Check Huu mfumo umeanzishwa tanzania kwa ajiri ya kuongeza kasi ya maendeleo kwa sababu itachochea kasi ya ukusanyaji kodi ya serikali lkn pia itaoingeza uwajibikajikati ya TRA, POLISI na Madereva wenyewe