Jinsi ya kurudisha uke uliolegea
Uke uliokuwa umelegea huleta hali ya kutojiamini na kutokuwa huru kwa wanawake wengi, na mara nyingi inahusishwa na mabadiliko ya kisaikolojia na kimwili. kama sio mwanamke ametoka kujifungua mtoto, hali hii humfanya mwnamke awe na wasiwasi na hayupo huru kukutana na mwanaume wake kwa kile anachohisi kwamba mwanaume wake atakiona, kama unavyojua wanaume wengi wanapenda uke unaobana na wanawake wanajua hilo.
Katika article hii tunaelezea kwa undani sababu za kulegea uke wa mwanamke na mambo ya kuzingatia ili kurudisha uke katika hali yake ya kawaida iwe mwanamke ametoka kujifungua au uke ulilegea kwa sababu nyionginezo ambazo zote tunazichambua hapa chini.
Kwanini Uke unalegea
Umri mkubwa
Mwanamke anapofika miaka ya 38 mara nyingi ataanza kuona utofauti kwenye misuli ya uke wake. Hii ni kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen. Kupungua kwa homoni ya estrogen kunafanya tishu za uke wako kusinyaa, kukauka na kutovutika. Hiki itakuwa ni kiashiria kwamba sasa umri umeenda sana na kuna uwezekano usiwe na uwezo wa kuzaa kama kawaida.
Pia soma: Jinsi ya kumvutia Msichana na Kumfanya Akutamani kimapenzi
Kujifungua mtoto/Kuzaa
Kupata mtoto kwa mara ya kwanza au ya pili na kadhalika kunachangia sana uke wa mwanamke kulegea sana, Ni jambo la kawaida kabisa kwa uke kulegea baada ya kuzaa,kwasababu misuli ya uke inatanuka sana ili kuruhusu mtoto kuzaliwa.
Hii ni kawaida na isikupe hofu kabisa. Uke wako utaanza kurejea katika hali yake ya kawaida siku chache baada ya kujifungua, japo hautarudi kama mwanzo. na hapo ndipo zinapoingia mbinu tyunazokupatia leo hakikisha unakuwa karibu na wikihii.com ili tuendelee kukupa mbinu za kujistiri nakubana uke ambao kuwa umetanuka kutokana na sababu mbalimbali kama tulivyosema hapo juu.
Mabadiliko ya homoni za kike
Mabadiliko ya homoni yanaweza pia kuchangia katika uke kulegea. Wakati wa kipindi cha menopause, viwango vya estrojeni hupungua, na kusababisha tishu za uke kupoteza unyumbufu na nguvu. Hali hii inaweza kuathiri uzalishaji wa majimaji ya uke na kusababisha ukosefu wa mvutano, hivyo kuleta hisia za kulegea. Mabadiliko haya yanaweza kuathiri afya ya kijinsia kwa ujumla na kuongeza hatari ya matatizo mengine.
Kukosa Mazoezi

Kukosa mazoezi ya mara kwa mara kunaweza kuathiri misuli ya pelvic na kusababisha kulegea kwa uke. Misuli ya pelvic inahitaji mazoezi ili kudumisha nguvu na unyumbufu wake. Kukosekana kwa mazoezi kunaweza kusababisha misuli ya uke kupoteza nguvu na uwezo wa kukaza, hivyo kupelekea hisia za kulegea.
Pia Soma: Mambo ya kuzingatia unapokuwa na mpenzi wako Usiku wa Kwanza
Mwanamke anatakiwa kuwa na ratiba ndogo ya mazoezi kidogo kwa siku hata ya kukimbia akiweza hii itafanya misuli ya uke kuchangamka na kurudi kwenye hali ya kawaidaWanawake wanapaswa kujumuisha mazoezi kama vile yoga au mazoezi ya Kegel katika ratiba zao za kila siku ili kusaidia kuimarisha misuli hii.
Magonjwa ya Kijinsia
Magonjwa kama vile fibroids, cysts, au magonjwa mengine yanaweza kuathiri tishu za uke na kusababisha kulegea. Uharibifu wa tishu hizi unaweza kuleta hisia za kutanuka na kusababisha wasiwasi. Ikiwa mwanamke anapata dalili kama vile maumivu au kutokwa na damu, ni muhimu kutafuta msaada wa kitaalamu. Magonjwa haya yanaweza kuathiri uwezo wa uke wa kujitunza na kusababisha mabadiliko katika muundo wake.
Jinsi ya kubana uke uliolegea
Mazoezi ya nyonga
Kwa mwanamke mambo yote muhimu yako kwenye nyonga hivyo ni muhimu kufanya mazoezi ya nyonga kwa sababu nyonga ndio amebeba uke tunaoujadili, mazoezi haya yatakufanya uanze kuwa na uimara katika misuli ya nyonga na nyonga yenyewe, anza kufanya mazoezi haya kidogo kidogo huku unaongeza kadri siku zinavyokwenda ndani ya muda mfupi sana utaanza kuona mabadiliko.
Mazoezi ya Kegel (Bana misuli ya uke)
Jaribu kufanya zoezi hili ukiwa unajisaidia haja ndogo peke yako wakati unakojoa jaribu kufanya kama unabana mkojo usitoke sekunde 5 halafu unauachia, unabana tena mkojo usitoke kwa sekunde kadhaa kabla haujauachia hakikisha unafanya hivi mara nyingi hadi inafika hatua unakua na uwezo wa ku control mkojo wakati unakojoa kawaida.
Ukifanikiwa kuweza kubana na kuachia mkojo basi tengeneza mazoea ya kufanya hivyo mara kwa mara kwa sababu hilo ni zoezi moja kubwa sana katika kusaidia kubana uke wa mwanamke nakuhakikishia ukiwa na mazoea ya kufanya hivi ukaigeuza hii ikawa ni utaratibu wako basi misuli ya uke wa mwanamke itakaza na uke pia utarudi kuwa mdogo kama bado ana bikra
Soma pia: Hizi hapa dalili za kukojoa kwa mwanamke mkiwa kwenye tendo.
Kama mwanamke atashindwa kufanya zoezi wakati wa kukojoa basi unaweza kujaribu njia ingine kwa kuingiza kidole ukeni mpaka ndani na ajaribu kubana misuli ya uke aone kama kidole kinabanwa. akifanya hivi mara 4 kwa siku inatosha.
Mazoezi ya Pelvic

Kukaza misuli ya uke wako kupitia zoezi hili fanya hivi simama wima na makalio yako yaegemee ukuta.vuta tumbo kwa ndani. Unapofanya hivi mgongo wako utanyooka kuelekea kwenye ukuta bana tumbo lako kwa muda wa sekunde 4 kisha jiachie fanya hivi mara 10 na awamu tano kwa siku nzima.
Kula chakula bora matunda na maji
Soma pia: Njia rahisi za kumfikisha mpenzi wako kileleni
Kula chakula bora pia ni njia mojawapo kukaza au kubana uke wa mwanamke lakini chakula kinatakiwa kuwa mlo kamili ukiambatana na matunda kama ndizi, machungwa, papai na mengine kama hayo, maji ya kunywa safi na salama yanasaidia kwenye mzunguko wa damu mwilini hivyo kusababisha mwili uendelee na utaratibu wake na hii inahusika moja kwa moja kwenye mfumo mzima wa uke wa mwanamke.
Punguza stress
Tunaweza kuhangaika kutafuta suluhisho la kitaalamu lakini kumbe baadhi ya wanawake stress ndio sababu uke kulegea moja kwa moja hata baada ya kujifungua uke haubani, unakuta mwanamke unastress mia mbili hamsini hapo uke utalegea tu kwa sababu ukiwa na stress huwezi kufanya mazoezi, huwezi kupangilia chakula bora na huwezi kuzingatia mambo ya afya.
Ikishindikana Muone daktari
Kuna baadhi wanawake matatizo yao ya uke yatatibiwa hospitalini kutokana na tatizo alilonalo mwanamke, achana na mambo ya uongo sijui kupaka limao au ndimu ukeni haya mambo yatakudhuru zaidi unaweza kujikuta uke unazidi kutanuka badala ya kubana, nenda kwa daktari muelezee shida ni nini then atakupa ushauri wa kitaalamu na ambao ni salama kwa afya yako.
Hitimisho
Sababu za uke kulegea ni nyingi na zinaweza kuwa na athari tofauti kwa wanawake. Ni muhimu kuelewa sababu hizi ili kuweza kutafuta ufumbuzi sahihi. Kwa kuzingatia mambo ambayo tumetoka kujadili kama vile mazoezi ya pelvic, mazoezi ya nyonga na mazoezi mengine, ushauri wa wataalamu, na hatua za kutibu, Wakati unakumbana na tatizo la uke kulegea, kumbuka kuwa si wewe peke yako, na kuna njia nyingi za kukusaidia. Usisite kuzungumza na wataalamu wa afya ili kupata msaada zaidi. Kila mwanamke ana haki ya kuwa na afya njema ya uke na kujisikia mtamu wakati wote
