Close Menu
wikihii.comwikihii.com
  • Home
  • Makala
  • Elimu
  • Biashara
  • Michezo
Facebook X (Twitter) Instagram
wikihii.comwikihii.com
  • Home
  • Makala
  • Elimu
  • Biashara
  • Michezo
Facebook YouTube WhatsApp
  • Home
  • Makala
  • Elimu
  • Biashara
  • Michezo
wikihii.comwikihii.com
Home » Elimu » Vyuo Vya Ualimu
Vyuo Vya Ualimu

Jinsi ya Kujiunga na Songea Teachers College: Ada, Fomu, Sifa na Kozi.

Updated:May 11, 20254 Mins Read
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Jinsi ya Kujiunga na Songea Teachers College Ada, Fomu, Sifa na Kozi Zinazotolewa
Jinsi ya Kujiunga na Songea Teachers College Ada, Fomu, Sifa na Kozi Zinazotolewa
Share
Facebook Telegram WhatsApp Copy Link

Jinsi ya Kujiunga na Songea Teachers College: Ada, Fomu, Sifa na Kozi Zinazotolewa

Songea Teachers College ni chuo cha serikali kilichopo katika Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma. Chuo hiki kilianzishwa mwaka 1927 na Wamisionari wa Kikatoliki wa Benedictine wa Peramiho, na baadaye kikanationalizwa mwaka 1970 kufuatia Azimio la Arusha la 1967. Tangu wakati huo, chuo kimekuwa kikitoa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya cheti na diploma kwa walimu wa shule za msingi.

Sifa za Kujiunga Songea Teachers College

Ili kujiunga na Songea Teachers College, muombaji anatakiwa kuwa na:

  • Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE) chenye ufaulu wa angalau D nne katika masomo yasiyo ya dini.
  • Kwa ngazi ya Diploma, muombaji awe na ufaulu wa Kidato cha Sita (ACSEE) wenye angalau alama moja ya principal pass na moja ya subsidiary pass, au awe amehitimu ngazi ya cheti (NTA Level 5) kutoka chuo kinachotambuliwa na NACTVET.
  • Umri usiozidi miaka 35 kwa waombaji wa mara ya kwanza.

Kozi Zinazotolewa Songea Teachers College

Songea Teachers College hutoa kozi zifuatazo:

  1. Basic Technician Certificate in Primary Education – NTA Level 4
  2. Technician Certificate in Primary Education – NTA Level 5
  3. Ordinary Diploma in Primary Education (Pre-service) – NTA Level 6

Jinsi ya Kupata Fomu ya Kujiunga Songea Teachers College

Fomu za kujiunga hupatikana kwa njia zifuatazo:

  1. Tembelea tovuti ya Wizara ya Elimu ya Tanzania: www.moe.go.tz
  2. Pakua Joining Instructions ya chuo kwa mwaka husika.
  3. Jaza fomu ya maombi kwa usahihi na ambatanisha nakala za vyeti vyako, picha ndogo (passport size), na risiti ya malipo ya fomu (kama ipo).
  4. Wasilisha fomu chuoni moja kwa moja au tuma kwa njia ya EMS/Posta.

Mahali Chuo cha Songea Teachers College Kilipo

Chuo kipo Songea Mjini, mtaa wa Matogoro Shuleni, takriban kilomita 4 kutoka stendi ya zamani ya mabasi. Usafiri unapatikana kupitia daladala, taxi (Tsh 5,000–10,000) au bodaboda (Tsh 1,000–2,000).

Mahitaji kwa Usajili Songea Teachers College

Utakapotua chuoni, hakikisha unakuja na:

  • Vyeti halisi na nakala 3 za kidato cha IV/Sita
  • Cheti cha kuzaliwa (original + nakala 3)
  • Fomu ya afya iliyojazwa hospitali ya serikali
  • Passport size picha 3 zenye background ya buluu
  • Picha moja ya mwili mzima ukiwa na sare ya chuo

Ada na Michango Songea Teachers College

Ada za Masomo Songea Teachers College (Makadirio)

Ada hutegemea kozi na ngazi husika, lakini makadirio ya kawaida ni kama ifuatavyo:

  • Cheti cha Awali (Basic Certificate): TZS 800,000 – 1,000,000 kwa mwaka
  • Technician Certificate: TZS 1,000,000 – 1,200,000 kwa mwaka
  • Diploma: TZS 1,200,000 – 1,500,000 kwa mwaka

Ni muhimu kuwasiliana na chuo moja kwa moja ili kupata viwango sahihi vya ada kulingana na mwaka husika.

  • Ada ya Mwaka: Tsh 450,000 (Tsh 225,000 kwa kila muhula)
  • Michango Mbalimbali: Tsh 200,400 kwa mwaka, zikiwemo:
    • NHIF (50,400)
    • Usafi, usajili, michezo, ulinzi, n.k.
    • Mahafali: Tsh 10,000

Sare ya Chuo Songea Teachers College

Wavulana:

  • Suti nyeusi 2, shati la ‘light blue’ 2, tai nyeusi, viatu vya ngozi, soksi nyeusi
    Wasichana:
  • Suti nyeusi 2 (sketi ya heshima), shati la ‘light blue’ 2, hijab (kwa Waislamu), tai ya kipepeo

Sare zote lazima ziwe na maadili ya ualimu — nguo za kubana, vitop, mitumba na sare za mtelezo haziruhusiwi.

Vifaa Muhimu vya Kuleta Songea Teachers College

  • Vifaa vya malazi: mashuka, blanketi, ndoo, mto, foronya, chandarua
  • Vifaa vya chakula: sahani, bakuli, kikombe, kijiko (si vya plastiki)
  • Kitaaluma: daftari quire 3 (10), kalamu, mathematical set, scientific calculator, vitabu vya TET
  • Koti jeupe kwa maabara, rimu 1 ya karatasi A4
  • Tsh 20,000 kwa mitihani

Afya

  • Lete fomu ya afya iliyojazwa
  • Kama una NHIF, lete kitambulisho chake. Kama huna, utachangia Tsh 50,400 kwa mpango wa wanafunzi.

Vifaa vya Usafi

  • Reki ngumu 1 na ufagio aina ya chelewa

Sheria na Kanuni za Songea Teachers College

Wanachuo wote wanatakiwa kufuata kanuni za mwenendo bora. Zitapewa rasmi siku ya usajili.

Mawasiliano:
Simu: 0759172182 / 0759168813
Tovuti: www.songeatc.ac.tz
Barua pepe: songeatc@moe.go.tz

Pata Orodha Kamili ya Vyuo vya Ualimu Tanzania – Ujiunge Leo!

Unavutiwa na taaluma ya ualimu? Je, unatafuta chuo kinachokufaa? Orodha yetu kamili itakusaidia kuchagua chuo bora cha ualimu. Pata taarifa muhimu kuhusu vyuo vya serikali na binafsi nchini Tanzania.

Vyuo Vyote Vya Ualimu Hapa

Hitimisho

Songea Teachers College ni chuo chenye historia ndefu ya kutoa walimu bora kwa shule za msingi nchini Tanzania. Ikiwa unatafuta chuo cha ualimu chenye mazingira mazuri ya kujifunza, walimu wenye uzoefu, na ada nafuu, basi Songea Teachers College ni chaguo sahihi. Fanya maamuzi leo kwa kuwasiliana nao na kuanza safari yako ya kuwa mwalimu bora wa Tanzania.

Jisajili leo!

Follow on Facebook Follow on YouTube Follow on WhatsApp Follow on Telegram
Share. Facebook Telegram WhatsApp Copy Link
Previous ArticleJinsi ya Kujiunga na Chuo cha Ualimu Kisanga Teachers College: Ada, Fomu, Sifa na Kozi
Next Article Jinsi ya kujiunga na chuo cha Ualimu Patandi Teachers College: Ada, Fomu, Sifa na Kozi

MAKALA ZINAZOHUSIANA

Sifa za Kujiunga Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS)

June 16, 2025

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS)

June 16, 2025

Jinsi ya Kuthibitisha Udahili Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS)

June 16, 2025

Jinsi ya Kutumia Muhimbili University E-Learning Portal

June 16, 2025

Ada na Gharama za Masomo Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS)

June 16, 2025

Jinsi ya Kuomba Hosteli Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS)

June 16, 2025
Biashara
Biashara

Makampuni Yanayouza Hisa ktk Soko la Dar es salaam Stock Exchange (DSE)

By Wikihii MediaJune 3, 20250

Makampuni Yanayouza Hisa ktk Soko la DSE – Dar es salaam Stock Exchange Uwekezaji katika…

Jinsi ya Kuagiza Bidhaa Kutoka Alibaba (China) Hatua kwa Hatua

June 3, 2025

Aina za mikopo CRDB Bank | Mikopo ya CRDB

June 3, 2025

Jinsi ya Kuomba Mkopo CRDB Bank

June 3, 2025

JINSI YA KUOMBA MKOPO NMB KWA WAJASIRIAMALI

June 3, 2025

Jinsi ya Kuomba Mkopo wa Halmashauri (10% kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu)

June 3, 2025

wikihii media

  • Disclaimer
  • Kuhusu wikihii
  • Sera ya faragha
  • Sheria ya Matumizi
  • Wasiliana na wikihii

Wikihii Services

  • Michezo
  • Forex Tanzania
  • Leo ktk Historia
  • Kipimo cha Mimba
  • Matokeo ya Mtihani

Wikihii Newsletter

Subscribe kwenye email list wikihii kupata Updates za Ajira punde tu Mara baada ya Ajira kutangazwa.

© 2025 wikihii.com Designed by Wikihii Media.
  • Cookies Policy
  • Wordpress Website Service

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.

Ad Blocker Enabled!
Ad Blocker Enabled!
Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors. Please support us by disabling your Ad Blocker.