Business Payments & Aggregation Manager
Business Payments & Aggregation Manager – Vodacom Tanzania (Julai 2025)
Vodacom Tanzania inawakaribisha wataalamu wenye motisha kubwa kujiunga nasi katika nafasi ya Business Payments & Aggregation Manager. Ukiwa sehemu ya timu yetu ya kimataifa, utakuwa mstari wa mbele katika kubuni suluhisho za malipo na ushirikiano wa kiteknolojia kwa kutumia nguvu ya M-Pesa kuimarisha ujumuishaji wa kifedha.
Majukumu Makuu
- Kuandaa na kusimamia mkakati wa jumla wa Aggregators wa Biashara na Malipo kuanzia ngazi ya kimkakati hadi utekelezaji wa kila siku.
- Kukuza mapato, kuongeza faida za njia za malipo, na kuimarisha nafasi ya soko kwenye huduma za aggregation na malipo kwa taasisi.
- Kubuni mifano mipya ya biashara ya ubunifu ndani ya mfumo wa Enterprise Aggregation & Payments ili kuongeza ushirikiano zaidi ya huduma za malipo za kawaida.
- Kusimamia juhudi za kitengo kufikia malengo ya kibiashara kwa kutumia teknolojia, ubunifu, na ushirikiano wa kimkakati.
Majukumu ya Kipekee
- Kusimamia utoaji wa huduma na kupanua wigo wa teknolojia kwa Aggregators wa ndani na nje.
- Kupanua mfumo wa malipo kupitia ushirikiano wa ticketing, pay bills, na majukwaa ya kimkakati.
- Kuboresha na kudigitalisha mchakato wa usimamizi wa Aggregators na uandikishaji wa wafanyabiashara wao.
- Kuhakikisha retention na uhamasishaji wa Aggregators waliolala au waliosita kutoa huduma.
- Kujenga mfumo wa teknolojia wa Aggregators unaowezesha fursa mpya katika ekosistemi ya malipo.
Sifa na Ujuzi Muhimu
- Ujuzi wa kuchambua data na kufanya maamuzi ya msingi wa takwimu.
- Uzoefu wa kukuza ushirikiano wa kimkakati na taasisi za Fintech, serikali au sekta binafsi.
- Uwezo wa kubuni huduma au bidhaa mpya kwa kuchanganua mapengo ya soko.
- Uzoefu wa usimamizi wa miradi migumu, michakato ya onboarding na mabadiliko ya kiteknolojia.
- Ufanisi katika mawasiliano, majadiliano na mauzo.
- Uwezo wa kufikiri tofauti na kuleta mapinduzi ya huduma.
Sifa za Kielimu na Uzoefu
- Shahada ya kwanza katika Biashara, Uchumi, Masoko au taaluma inayohusiana.
- Uzoefu wa angalau miaka 5 katika kampuni kubwa, ikijumuisha angalau miaka 3 katika sekta ya Mawasiliano, Benki, FMCG au Fintech.
- Utaalamu katika mikakati ya majukwaa ya kidigitali, Aggregation Models au B2B2C Ecosystems.
Nafasi Kwa Watu Wote
Vodacom inathamini utofauti na usawa. Kama unahisi una uwezo wa kuchangia kwa nafasi hii hata kama huna vigezo vyote vilivyoorodheshwa, bado unakaribishwa kuomba. Tunaamini watu tofauti huleta matokeo bora.
Faida za Kujiunga na Vodacom
Vodacom ni zaidi ya kampuni ya mawasiliano – ni sehemu ya maisha ya watu. Tunakuza ujumuishaji, tunahamasisha maendeleo, na kuunganisha dunia kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa lengo la kuboresha maisha ya watu na mazingira yao.
Jinsi ya Kuomba
Kama una nia ya kuchukua hatua inayofuata katika taaluma yako, tafadhali tuma maombi yako kupitia kiungo kilicho hapa chini:
Aina ya kazi: Muda Wote (Full-Time)