Biashara ya forex imeendelea kubadilisha maisha ya watu wengi ambao wameichukulia serious kwa bahati nzuri ninaandika mimi mwenyewe nikiwa na uzoefu wa takriban miaka 7 katika hii biashara ya trading, Nimeona watu wengi wakitoboa na wengine wakifilisika kwa sababu ya hii forex, sasa relax kwenye hii article naenda kukuelezea basics za biashara ya forex na jinsi ya kufanya forex kama kazi na kujitengenezea kipato kama sio kubadilisha maisha yako kabisa.
Kwa taarifa tu forex ni biashara inayoongoza kwa kuwa na mzunguko mkubwa wa pesa inakadiriwa soko la forex linazungusha takriban trilioni saba (7) kwa siku moja hichi ni kiasi kikubwa sana cha pesa hii inamaanisha kwenye hii biashara kuna pesa ukiwa na nia ya kufanya forex.
Table of content
Unafanya vipi forex na Unapataje faida kwenye forex
Naamini wewe unayesoma hapa unazifahamu pesa na unafahamu kwamba kila nchi wanatumia pesa halisi za nchi zao, sasa kitendo cha kubadilisha pesa ya nchi moja kwenda pesa ya nchi nyingine hichi kitendo ndio forex ktk maana ya kawaida kbs, mabadilishano haya ya pesa za kigeni yanaweza kusababishwa na sababu za kibiashara, sababu za kitalii, au sababu nyinginezo (zipo nyingi).
Sasa forex tunayoizungumzia hapa leo sio hiyo ya Physical (kubadilisha pesa bank, bureau de change), hapa tunazungumzia forex ya online tunaifanya kupitia platform maalum kama vile Metatrader4, Metatrader5 au Tradingview, na tunatumia madalali wa forex (brokers) maalum kununua na kuuza pesa za nchi mbalimbali (currency trading -forex).
Kwenye masoko ya forex bei zinapanda na kushuka mara kwa mara kitendo hichi kwenye trading tunakiita market volatility na kimsingi hapo ndipo forex trader anapoweza kutengeneza pesa akiwa na maarifa ya forex trading kwa sababu forex tunaifanya kwa kufanya mambo mawili tu kuuza na kununua (buy and sell), swali linakuja unauza wakati gani?, au unanunua wakati gani?, majibu yako unayapata kwenye paragraph inayofuata.
Mpango mzima kwenye forex ni kwamba unanunua pale unapohisi bei itapanda – ikipanda kweli unapata faida wakati huohuo kama bei ikishuka unapata hasara, Lakini pia unauza pale unapohisi kwamba bei itashuka -ikishuka kweli unakuwa unapata faida na wakati huohuo ikiwa inapanda unakuwa unapata hasara.
Kinachotakiwa kwenye hii biashara ya forex ni kufanya predictions sawasawa, kwa sababu kitu pekee ambacho ni naamini ni kweli ni kwamba bei ikienda upande wako kama umenunua au umeuza basi unapata faida tena kadri bei inavyozidi kwenda upande wako wa mtaji wako unakuwa unaendelea kupanda direct kwenye metatrader platforms.
Kitu kimoja twende sawa ninaposema prediction au kuhisi kama bei itapanda au itashuka hii sio bahati nasibu, na wala sio betting, kwenye forex tunahisi bei itapanda au kushuka kwa kutumia mbinu zake maalum za kitaalamu na nyingine za kiuchumi zinazotambulika kufanya uchambuzi kwenye masoko ya forex,
Bofya kutumia Forex Tools
Tembelea pages zetu za Forex – kama Kalenda ya Uchumi, Viwango vya fedha, Pips Calculator, Position Size Calc, Lot Size Calc, Time Zone (Market Hours)
Fungua Forex ToolsMaana ya Forex pairs
Kwenye forex tunachotrade hasa ni pairs, mfano wa pair ni kama GBPUSD, EURUSD, XAUUSD, USDJPY na nyingine nyingi cha msingi hapa ni kwamba kuna MINOR PAIRS na MAJOR PAIRS, yaani pairs kubwa na ndogo,
Tuchukulie mfano wa GBPUSD PAIR – hii ni pair ambayo inajumuisha pesa za nchi mbili tofauti kuna GBP ambayo ni kifupi cha British Pound, halafu kuna USD ambayo ni kifupi cha United States Dollar, Pesa au currencies hizi mbili zinatrade against each other, yani GBP akiwa anapanda wakati huohuo USD anakuwa anashuka na Viceversa its true.
Soma Hii: BIASHARA YA FOREX PDF
Kupanda au kushuka kwa bei katika soko lolote kunasababishwa na mambo mengi inaweza kuwa news, inaweza kuwa sera za benk kuu ktk nchi husika, inaweza kuwa hali ya vita au matukio mengine yanayoweza kuathiri masoko ya currencies (forex), Soko la forex linafanya kazi siku 5 za wiki hii ina maana masoko ya forex hayafanyi kazi weekend.
Session zilizopo kwenye forex
Kuna masoko mbalimbali ya kidunia ya forex hapa sasa nazungumzia market sessions, hapa tuna masoko makubwa manne duniani kote ambayo ni LONDON SESSION, NEWYORK SESSION, SYDNEY SESSION na TOKYO SESSION.
Hizo session hapo juu ndio ufunguo wako kwa sababu hizo session ndio zinakuonesha kwamba mabenk ya United Kingdom (UK) sasa yamefunguliwa ikiwa ni London session, au Mabenki ya USA sasa yamefunguliwa ikiwa ni NY session na kadhalika wakati huohuo kwenye trading tunatakiwa kufanya bishara wakati ambao traders wengi wapo live online kwa sababu tunahitaji Volume ya traders wakiwa wengi maana yake kutakua na nguvu kubwa ya kuweza kupush na kwenda uelekeo fulani (uptrend, Downtrend).
Soko la forex lipo huru mtu yeyote anaweza kufanya trading kinachotakiwa ni PC/Laptop yako na access ya internet everytime, lakini sasa ni wakati wa kuwajua wahusika wakubwa kwenye masoko ya forex hapa namaanisha watu au makampuni ambayo nayo yanaishi kwa kufanya forex trading kama ambavyon wewe unayesoma hii makala unatamani kuishi kwa kufanya forex Wahusika wakubwa ni Benki mbalimbali, Makampuni yanayofanya kazi ya ku manage mitaji mikubwa kitaalamu tunayaita HEDGE FUNDS MANAGEMENT COMPANIES, Forex Brokers wenyewe, Serikali yoyote ile itahusika kwenye forex kupitia sera mbalimbali za kiuchumi au kupitia benki kuu ambayo inajulikana kwa uwezo wake wa kushusha au kupandisha interest rate (riba) ambayo hupelekea volatility kubwa sana kwenye soko husika.
Bofya kutumia Forex Tools
Tembelea pages zetu za Forex – kama Kalenda ya Uchumi, Viwango vya fedha, Pips Calculator, Position Size Calc, Lot Size Calc, Time Zone (Market Hours)
Fungua Forex ToolsPlatform zinazotumika kwenye forex
Kwenye trading tunatumia platforms maalum kwa ajiri ya ku trade hapa namaanisha METATRADER4 (MT4) na METATRADER5 (MT5) Hizi ni platform maalum kwa ajiri ya kuingia na kutoka kwenye trade pamoja na kufanya trade management kuweka Stop Loss, Take profit na kadhalika, Lakini ili tufungue trade (position) tunatakiwa kuwa na account real kutoka kwa dalali wa forex (BROKER) hapa kuna machaguo mengi hawa forex brokers wapo wengi sana kwa mfano kuna TD365, FBS, XM, EXNESS List inaendelea kwa sababu wapo wengi sana cha kuzingatia hapa ni kwamba kila broker anatofautiana na mwingine interms of services offered, kwa hiyo ni vzr kusoma na kuelewa conditions a broker kama zitakufaa kabla ya kufungua account na broker huyo,

Utahitajika kuverify account yako hivyo lazima uwe na vitu kama Kitambulisho (NIDA,PASSPORT YA KUSAFIRIA AU LESENI YA DEREVA), Pia kitu kingine muhimu ni Kitambulisho cha makazi hapa unaweza kutumia Kitambulisho cha mkazi chenye muhuri kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa wako, au kama tayari unayo bank account basi unaenda kuchukua bank statement hii wanaverify mapema sana, kama hauna kitu kingine kinachoweza kuverify makazi yako ni bili za maji au umeme zenye jina lako au jina lililopo kwenye kitambulisho ulichowasilisha.
Forex basics | Namna Masoko yanavyozunguka
Kwenye masoko yoyote yale ile forex, stocks au Indices yote yanaoperate kwa jinsi hii sokoni kuna watu wanaonunua (Buyers) na waatu wanaouza (Sellers), wanaonunua ambao ni buyers wakinunua kuwazidi wanaouza ambao ni sellers Bei INAPANDA. Viceversa is true watu wanaouza wakiuza sana kuwazidi wanaonunua ambao ni buyers Bei INASHUKA.
Hivyo ndivo buyers na sellers wanavyolizungusha soko la forex na kumbuka tunavyosema buyers na sellers tunamaanisha BIG BANKS, HEDGE FUNDS, TRADING COMPANIES na Players wengine sokoni ambao wanatrade kiasi kukubwa cha pesa halafu kuna mimi na wewe (RETAIL TRADERS) tunatrade kupitia Madalali wa forex (BROKERS) tunatrade wakati wowote kwenye PC/PHONE kwa sababu ya zile platform nilizozungumzia mwanzoni (MT4, MT5) pamoja na broker mwenyewe.
Bofya kutumia Forex Tools
Tembelea pages zetu za Forex – kama Kalenda ya Uchumi, Viwango vya fedha, Pips Calculator, Position Size Calc, Lot Size Calc, Time Zone (Market Hours)
Fungua Forex ToolsMbinu za kufanya uchambuzi kwenye masoko ya forex
Mpaka sasa nadhani tumeshaelewa kwamba tunapata pesa Bei ikienda upande wetu (PROFIT) na tunapata hasara Bei ikienda upande ambao sio wetu (LOSS) sasa inshu kubwa kwa trader ni kujua kama Bei itapanda au itashuka hapa ndio kwenye mpango wenyewe kwa sababu ukigundua kama Bei itapanda maana yake utanunua (BUY) na ukigundua Bei itashuka maana yake Utauza (SELL), Challenge kubwa kwenye forex ni kugundua kama Bei itapanda au Itashuka na Hapo ndipo zinapokuja mbinu mbalimbali za kufanya forex
Kuna Mbinu nyingi sana zinazotumika kuchambua masoko ya forex lakini muhimu ni kwamba katika mbinu zote hizi zimegawanyika katika Mbinu za Fundamental na Mbinu za Kitaalamu.
Mbinu za Fundamental: ni zile mbinu zote ambazo zinaangalia sababu za kiuchumi kwa mfano sera za bank kuu ktk nchi fulani, namba za ajira ktk nchi, ukuaji wa uchumi, vitu kama Gross Domestic Product (GDP), Interest Rate/Riba, Balance of trade au namna jinsi nchi inavyofanya biashara na nchi nyingine (Imports na Exports), Hapo pia kuna FOREX CALENDAR (NEWS) hizi ni taaarifa za kiuchumi za nchi mbalimbali ambazo zinaonesha siku na muda ambao tukio (news) itatangazwa.
Mbinu za Kitaalamu: Ni zile mbinu zote ambazo zinaangalia Utaalamu wa kutafuta levels, Momentum, Volume, pamoja na matumizi ya Indicators mbalimbali the like of RSI, MACD na nyinginezo, Pia kuna Mbinu mbinu za kitaalamu zinazotusaidia kuangalia movement za soko (price action) kiukweli kwenye hii category ya technical kuna mbinu nyingi sana tukizihesabu ni kama vile Demand & Supply, Support & Resistance, Breakout strategy, Pullback strategy, Fading strategy, Liquidity strategy na list inaendelea kama nilivyosema nikisema nizitaje hatuwezi kumaliza.
Itaendelea…..