Usaili wa Maafisa wa Kura Uchaguzi 2025
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inaendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo.
NEC imetangaza rasmi wito wa usaili kwa waombaji waliokuwa na nia ya kushiriki kama Maafisa wa Kura katika vituo vya kupigia kura kote nchini. Zoeezi hili ni muhimu kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, uwajibikaji, na uadilifu.
Taarifa hii inatolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 6(6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Nambari 1 ya mwaka 2024, pamoja na Kanuni ya 11 za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2025. Hii inahakikisha kuwa watumishi wa vituo vya kupigia kura ni wataalamu, wa haki, na wanaoweza kuendesha uchaguzi huru na wa haki.
Kwa maelezo zaidi na mchakato wa usaili katika halmashauri zote, hakikisha unatembelea post yetu ya kina.
