Biashara ya forex jamii forum
Forex ni biashara ambayo inafanywa na watu wenye maarifa na kwa bahati nzuri jamii forum imeendelea kuwa jukwaa muhimu kwa watu wenye maarifa mbalimbali nchini tanzania kwa miaka mingi sana, jamii forum kuna articles nyingi sana zilizoandikwa na watu mbalimbali wenye maarifa ya trading,
Kwanini watanzania wengi wanafeli kwenye masoko ya forex
Vijana wengi Wanafeli kwa sababu ya ushawishi wa watu wanaowafundisha forex, wanaofanya forex ionekane ni nyepesi ukiwa trader na kwamba fedha zinapatikana kwa urahisi sana kwenye forex kitu ambacho sio kweli.
Watu wanaingia kwenye huu mtego na kuvamia hii fani bila utafiti wowote huku wakiwa na expectation kubwa sana za kupata fedha za bwerere.
Kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu forex na pia kutofanya practice ya kutosha ili kupata uzoefu wa kutrade forex ikiwemo kujenga trading strategy pamoja na displine ya kutrade. Hata kwenye industry nyingine huwezi kutoboa kirahisi rahisi tu. Watu wote ambao ni successful katika career zao wamepambana sana sana mpaka kufikia hapo walipo sasa.
Mtaji mdogo pia ni sababu ya watu kupoteza fedha kwani kuwa na mtaji mdogo kunawafanya traders wengi kuwa aggressive (overtrading & poor risk management) na hivyo kutofuata taratibu/rules za kutrade forexx na mwisho wake wanaishia kupoteza fedha. wanatrade kwa shinikizo kubwa la kupata hela
Wenye mitaji mikubwa wanaopoteza fedha ni kwa sababu tu ya kuwa GREEDY au kutofuata risk management rules au kutokuwa na elimu au uelewa wa kutosha kuhusu forex, au kutokuwa na strategy nzuri za kutrade forex..
Kwa ujumla FOREX inaweza kukupa fedha za kutosha tu kama utapata elimu sahihi, utapractice sana na kuwa na strategy inayofanya kazi vizuri, utafuata risk management rules na pia ukiwa na mtaji mkubwa ni faida ya ziada advantage ya kukufanya upate profit kubwa endapo utakuwa na maarifa sahihi ya jinsi ya kufanya forex trading.
Historia ya forex market
Katika mwaka 1971, Marekani iliachana na mfumo wa Bretton Woods uliokuwa unashikilia thamani ya dola ya Marekani kwenye dhahabu. Hii ilisababisha mfumo wa ubadilishaji wa fedha za kigeni kufunguliwa na kuruhusu sarafu kubadilishwa kwa thamani ambayo ilikuwa inategemea nguvu ya soko.
Teknolojia ya kompyuta ilichochea ukuaji wa soko la forex kwani mifumo ya elektroniki iliwezesha mawasiliano ya papo hapo na shughuli za biashara ya fedha duniani kote. Kuanzia miaka ya 1990, internet ilianza kuingia kwa kasi na kuongeza upatikanaji wa soko la forex kwa watu binafsi (Retail Traders).
Bofya kutumia Forex Tools
Tembelea pages zetu za Forex – kama Kalenda ya Uchumi, Viwango vya fedha, Pips Calculator, Position Size Calc, Lot Size Calc, Time Zone (Market Hours)
Fungua Forex ToolsLeo hii, forex imekua kiasi kwamba ndio baishara pekee duniani ambayo mzunguko wake wa fedha kwa siku ni zaidi ya trilioni 7 Watu binafsi, makampuni, na benki hujiingiza katika biashara ya forex ili kufaidika na tofauti za thamani za sarafu mbalimbli na hivyo watu wenye maarifa hutengeneza pesa hapa.
Kwanini sitaacha forex (Manufaa ya trading)
Uwezo wa Kupata Faida: Forex ni soko kubwa linalofanya kazi masaa 24 siku 5 za wiki (24/5), ambalo linatoa fursa nyingi za kuweka biashara na kupata faida. Faida inaweza kupatikana kutokana na mabadiliko madogo ya bei katika pair mbalimbali za fedha mfano EURUSD, GBPUSD, XAUUSD nk.
Urahisi wa Kuingia na Kutoka: Soko la forex lina uwazi na urahisi wa kuingia na kutoka. Hii inamaanisha kuwa unaweza kufungua na kufunga biashara kwa urahisi wakati wowote unaofaa kwako, hapa namaanisha ENTRIES na EXITS,
Uwezo wa kuuza au kununua: Katika soko la forex, unaweza kufanya biashara katika mwelekeo wowote, yaani, unaweza kununua au kuuza pair ya fedha. Hii inamaanisha kuwa unaweza kuchukua faida kutokana na kupanda kwa bei (kununua) au kushuka kwa bei (kuuza).
Uwekezaji wa Kimataifa: Forex hutoa fursa ya kuwekeza katika sarafu za nchi tofauti na kuchukua faida kutokana na tofauti za kiuchumi na kisiasa kati ya nchi hizo. Lakini pia kwenye stocks unaweza kumiliki hisa za COCACOLA hata kama unaishi BUZA kupitia masoko ya fedha (forex)
Leverage ya Broker: Katika masoko ya forex, traders waliofungua account na kuverify kwa broker wanapatiwa mkopo (Leverage) kutoka kwa broker hii inatuwezesha kuingia au kufungua position hata kama mtaji ni mdogo, na kama ukiwa na maarifa hivi vyote ni advantage kwako wewe.
Mambo ya kuzingatia ili usije kuichukia forex
1. Hatari ya Kupoteza Fedha: Biashara ya forex ni hatari na kunaweza kuwa na uwezekano wa kupoteza fedha zako. Bei ya pair za fedha inaweza kubadilika kwa haraka na imetawaliwa na mambo mengi kama habari za kiuchumi, siasa, na matukio ya kimataifa. Hivyo, kuna hatari ya kupoteza fedha yako ikiwa hautafanya uchambuzi sahihi na kutumia mbinu za usimamizi wa hatari.
2. Uvumi na Habari (Fake News): Soko la forex linaweza kuvurugwa sana na fake news. Uchambuzi mzuri uliozingatia sababu za kiuchumi pamoja na technical strategies unahitajika ili kupata habari sahihi, kuepuka kuzama kwenye fake news ambazo zinaweza kukusababishia hasara kubwa.
Matukio ya kidunia (Global Trends): Soko la forex linaweza kubadilika kwa ghafla kutokana na masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, na kijiografia. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha impact kwenye masoko ikapelekea bei kushuka au kupanda kwa nguvu.
MANIPULATIONS: Kama kuna kitu muhimu trader anatakiwa kukizingatia basi ni trading manipulations hii imekaa kitaalamu zaidi lakini kimsingi ni namna ambavyo mabenki wanatrade dhidi ya sisi (retail traders) na kutokana na uwezo wa pesa walionao ni ngumu kushindana na hawa MARKET MAKERS.
Bofya kutumia Forex Tools
Tembelea pages zetu za Forex – kama Kalenda ya Uchumi, Viwango vya fedha, Pips Calculator, Position Size Calc, Lot Size Calc, Time Zone (Market Hours)
Fungua Forex Tools