WITO WA USAILI ZIMAMOTO – FIRE AND RESCUE FORCE (DESEMBA 2025)
Tarehe ya Tangazo: 12 Desemba 2025
Utangulizi
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anawatangazia vijana wote walioomba ajira kupitia mfumo rasmi wa ajira.zimamoto.go.tz kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 15 Desemba 2025 hadi 20 Desemba 2025, kuanzia saa 1:00 asubuhi kila siku.
Ratiba ya Usaili kwa Makundi Tofauti
Waombaji wa Elimu ya Kidato cha Nne (Form Four)
Waombaji wote waliomba nafasi zinazohitaji elimu ya Kidato cha Nne watafanya usaili:
- Tarehe: 15 Desemba 2025
- Muda: Kuanzia saa 1:00 asubuhi
- Mahali: Katika mikoa waliyowasilisha maombi yao
Waombaji wa Astashahada (Diploma) na Shahada (Degree)
Waombaji wa ngazi ya Diploma na Degree watafanya usaili katika:
- Mahali: Ukumbi wa Andengenye – Makao Makuu ya Zimamoto, Dodoma
- Tarehe: 15 hadi 20 Desemba 2025
- Muda: Kuanzia saa 1:00 asubuhi
Makundi ya Kada na Ratiba Zake
a) Kada za Michezo (Sportsmen)
- Kundi A – 15 Desemba 2025
- Kundi B – 16 Desemba 2025
- Kundi C – 17 Desemba 2025
Makundi yameainishwa rasmi kwenye tovuti ya Zimamoto.
b) Emergency Medical Technician na Nursing
- Tarehe: 18 Desemba 2025
c) Diving
- Tarehe: 19 Desemba 2025
d) Kada Nyingine za Kitaaluma
Usaili wa kada zifuatazo utafanyika tarehe 20 Desemba 2025:
- Fire Fighting and Rescue Profession
- Avionics
- Civil Engineer
- Data Scientist
- Motor Vehicle Mechanics
- Quantity Surveyor
- Marine Engineer
- Oil and Gas Engineer
- Office Management Secretary
- ICT Technician
- ICT Network Technician
- Madereva (Drivers)
Masharti Muhimu kwa Washiriki wa Usaili
- Kila mwombaji anatakiwa kufika kituo cha usaili kwa tarehe aliyopangiwa.
- Kila mwombaji lazima alete vyeti halisi (ORIGINAL) vya elimu kuanzia Form Four, Form Six, na vyeti vya kitaaluma.
- Cheti cha kuzaliwa na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA ni lazima.
- Waombaji wa nafasi za udereva waje na leseni halali ya daraja la Class E.
- Gharama zote za usafiri, chakula na malazi zitagharamiwa na mwombaji mwenyewe.
Orodha ya Waliochaguliwa (Shortlisted)
Orodha kamili ya waombaji waliochaguliwa kwa ajili ya usaili pamoja na makundi yao inapatikana kupitia tovuti rasmi ya Jeshi la Zimamoto:
Viungo Muhimu vya Ajira
- Ajira mpya za Zimamoto na taasisi nyingine: Wikihii
- Ajira mpya Tanzania (Jobs Updates): Bonyeza hapa
- Jiunge na Channel ya WhatsApp kwa taarifa za ajira: Wikihii Updates
Hitimisho
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linawahimiza waombaji wote waliochaguliwa kuzingatia ratiba, kufika mapema, na kubeba nyaraka zote muhimu kwa ajili ya usaili. Hii ni fursa muhimu ya kujiunga na taasisi nyeti ya ulinzi na usalama wa raia wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kamishna Jenerali
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu – Dodoma
Pakua Tangazo Kamili (PDF): DOWNLOAD FULL PDF HAPA

