Madhara ya punyeto kiislamu
Punyeto au kujichua ni kitu ambacho kimekatazwa na kimezungumziwa mmara kadhaa kwenye quraan Kujichua wanaume au kujisaga wanawake ni jambo linalokubalika na kufanyika sana katika mataifa ya west na watu ambao sio waislamu Kiislam kwa idadi kubwa ya watu: vijana wa kiume na kike, makapera, wazee na hata waliooa/kuolewa.
Katika Uislam ni kinyume na maadili n autaratibu aliotuachia mtume muhammad. Kwani katika Uislam kujichua au kujisaga (punyeto) ni haraam kwa mwanamme na mwanamke, Jambo hili limezungumziwa katika Quraan
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٥﴾إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٦﴾فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿٧﴾
Na ambao wanazihifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume basi hao hawalaumiwi. Lakini atakayetaka kinyume ya hayo; basi hao ndio wapindukao mipaka.
[Al-Muuminuwn: 5-7]
Aayah hii inakataza waziwazi vitendo vyote vya tendo la ndoa (ikijumuisha punyeto) isipokuwa kwa wake, na yeyote anayejipelekea kwenye matendo kinyume na hayo yaliyoruhusiwa, basi ni katika warukao mipaka.
وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ
Na wajisitiri (yaliyoharamishwa) wale ambao hawapati uwezo wa ndoa mpaka Allaah Awatajirishe katika fadhila Zake. [An-Nuwr: 33]
Aayah hii vilevile inaamrisha wazi kwa yule asiye na uwezo wa kimali kwa ajili ya kuoa, basi anatakiwa ajiweke katika hali ya kujidhibiti na machafu na kujihifadhi kimwili na awe na subira ya kuweza kukabiliana na vishawishi mbalimbali ikiwemo kupiga punyeto, hadi Allaah Atakapomruzuku kwa fadhila Zake.
Vilevile Wanazuoni wa Fiqh (Fuqahaa) wamechukulia hukumu kutoka katika ayah hii kuwa ni haraam kupiga punyeto kwa sababu mbili: Ya kwanza: Katika ayah hii, Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa Anaamrisha kujizuia na machafu, na kutokana na kanuni za ki-Fiqh, maamrisho yanaashiria ulazima (uwajibu) wa jambo.
Hivyo kubaki katika hali ya usafi (kujizuia na machafu) ni wajibu na panapokuwa kujizuia na machafu ni wajibu, basi kujizuia na yale yote yanayopelekea kufanya machafu ni wajibu zaidi. Hii inatokana na ukweli kwamba kujizuia na machafu au kubaki safi kutapatikana pale mtu anapojizuia na vile vyenye kusababisha hayo machafu.
Soma Hii: Tiba ya madhara ya punyeto
Sababu ya pili, kwamba katika ayah hiyo Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa Ameamrisha Usafi (kutofanya machafu) kwa wale wasio na uwezo wa kuoa. Hapa Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa Hajadhihirisha uhusiano wa kujizua na machafu na ule wa kuoa. Hivyo kunahesabika kuwa kujichua ni haraam.
Na kama kungekuwa ni halaal, basi hapa ndipo pahala pake palipokuwa panatakikana kutajwa. Kwa kutotajwa uhalali wa kujichua katika ayah hii ambapo ndipo pahali muwafaka wa kuelezwa hilo, kunadhihirisha kuwa jambo hilo ni haraam, Kwani ‘kunyamazwa katika sehemu ya kuelezwa kunaashiria makatazo.’ Tazama pia tafsiri ya Imaam Qurtubiy katika aayah hiyo.
Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam) amesema:
((يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ مَنْ اسْتَطَاعَ الْبَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ فَإِنَّهُ أَغَضُّ لِلْبَصَرِ وَأَحْصَنُ لِلْفَرْجِ وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَهُ وِجَاءٌ)) البخاري ومسلم
((Enyi vijana, anayeweza kuoa basi na aoe kwani ni kuinamisha macho na ni stara ya uchi, Na asiyeweza basi afunge (Swawm) kwani ni kinga (ya matamanio).[Al-Bukhaariy na Muslim]
1. Kuutumia muda wako usio na la kufanya, kwa kufanya ibada zaidi na kujisomea na kutafuta elimu ya dini; kwa kusikiliza mawaidha au kutazama.
2. Kujiepusha na kutumia baadhi ya vyakula, vinywaji n.k. ambavyo vinachochea hamu na kusababisha mshawasha na muibuko wa matamanio.
3. Daima fikiria madhara yanayoweza kusababishwa na tendo hilo; kama ya kudhoofisha nguvu za macho, nguvu za mishipa, nguvu za uume (kwa mwanamme) au uti wa mgongo. Na muhimu zaidi, ni kule kuwa na hisia za dhambi na usumbufu utakaopatikana baada ya kufanya kitendo hicho kama vile, kuweza kupoteza Swaalah ya faradhi kwa kukubidi kuchukua muda wa kwenda kuoga kila baada ya tendo hilo.
4. Fanya Tawbah, muombe Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) msamaha kila wakati, kufanya hivyo na pia kutenda matendo mema na kutokata tamaa na Rahma za Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa kunaweka karibu zaidi na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kukufanya kumuogopa zaidi na kufikiria kila tendo unalotaka kulifanya kwanza.
Soma Hii: Vyakula vinavyotibu madhara ya punyeto
5. Jua kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni Mwingi wa Kusamehe na daima Humkubalia du’aa za yule anayemtaka msaada. Hivyo basi, kumuomba Allaah(Subhaanahu wa Ta’aalaa) msamaha ni jambo lenye kupokelewa Naye, na hilo linatupa nguvu kumuomba Yeye daima na kutaraji msamaha Wake.
6. Kujishughulisha na mambo ya muhimu na ya faida; yakiwa ni ya akhera au ya kilimwengu ili usipate nafasi ya kuwa na faragha na ukaanza kufikiria kufanya tendo hilo ambalo hakika ni ada iliyo ngumu kuepukika.