Jinsi ya kuwa na baby face
Mwanaume mwenye muonekano wa baby face huwa anawavutia wasichana wengi sanakwa bahati mbaya kutokana na shughuli mbalimbali za maisha wanaume tunapigwa sana na jua kwenye harakati zetu za utafutaji hali inayopelekea sura kukunjamana (makunyanzi) sasa habari njema ni kwamba kuna mbinu za asili (NO CHEMICALS) ambazo ni salama kuzitumia na kurudisha uso wako katika hali ya kawaida.
Kuna njia nyingi za kusafisha uso wako uonekane wa kuvutia na kupendeza. kwenye hii article tunaenda kuangalia mbinu za kusafisha uso kwa njia ya asili. Njia za asili ni bora kuliko hizo kemikali wanazotumia wanawake wengi, ukitumia njia za asili means hakuna madhara yeyote yale yatakayosababishwa.
Njia hii ni simple tu kwamba ni kwamba anza utaratibu maalumu ndni ya mwezi mmoja tu ndani ya huu mwezi kila siku kabla ya kulala unajipaka mchanganyiko ambao naenda kukuelezea soon! lkn unatakiwa unajipaka na unakaa na huu mchnganyiko kwa takriban nusu saa kabla ya kwenda kuosha na maji ya uvuguvugu.
MCHANGANYIKO
Mchanganyiko wetu ni maji ya uvuguvugu unayachanganya na Asali, Sukari, Maziwa yasiyowekwa maji, na Limao au Yai la Kuku wa kienyeji (ile njano yake). zingatia vipimo hivi ambapo kwa maji lita 5 utatumia kijiko kimoja cha Asali, vijiko viwili vya sukari, Maziwa kikombe cha kahawa, Limao moja unaminyia lote, Hakikisha unavuruga/changanya mchanganyiko huu hadi rangi inakua ya kama njano flani hivi hapo inakua tayari kwa matumizi.
Soma Hii: Jinsi ya kuwa na uso soft
MATUMIZI YA MCHANGANYIKO
Jinsi ya kutumia mchanganyiko huu ni very simple baada ya kuchanganya dawa yako kabla ya kulala unapaka usoni kisha unaacha kwa dakika 25 hadi 30 ndipo utasafisha uso wako tena kwa kutumia kitambaa safi na maji ya uvuguvugu tena lakini yasiyochanganywa mchanganyiko wa dawa yako, hakikiaukimaliza zoezi hili moja kwa moja unaenda kulala kuipa nafasi dawa ya asili iliyopo kwenye mchanganyiko ifanye kazi, Sio unapaka mchanganyiko kisha unaenda BAA.
Iwe una ngozi kavu haina mafuta au imekakamaa huu mchanganyiko utailainisha ngozi yako na itarudi kuwa soft tena kama ulivyokuwa mtoto.