Toyota Alphard ni gari linalovutia kwa muundo wake wa kifahari na wakuvutia ambao umekua kwa kasi tangu lilipoanzishwa. Gari hili lilianza kuzalishwa mwaka 2002 na limekua likipata muundo mpya hadi mwaka 2023. Alphard inalenga zaidi kwenye soko la watu ambao wanapenda gari za kifahari na zenye nafasi ya kuweza kubeba abiria wengi ndani, ni gari inafaa kwa shughuli za kitalii (kuwatembeza watalii town trip). lakini pia gari inafaa kwenye shughuli za hoteli food delivery, hata kubeba maharusi kutokana na jinsi lilivyokua la kifahari na lina nafasi kubwa.

Toyota Alphard inasimama kama chaguo bora kwa familia kubwa na makundi yanayohitaji kutembea pamoja inaweza kuwa kampuni, project fulani au just trip tu yenye lenggo lolote lile ukiwa unataka gari itakayoweza ku accommodate watu wengi kwa pamoja basi Alphard ni chaguo bora sana.
Toyota Alphard imejidhihirisha kwa ubora wa teknolojia ya kiufundi ulioboreshwa sana, ikiwa na injini zenye nguvu za kuanzia cc 2.4 hadi 3.5, ambazo hutoa uwezo wa nguvu na matumizi ya kawaida ya mafuta. Muhimu zaidi ni teknolojia za kiusalama zilizowekwa, kama mfumo wa braking za kisasa na airbags nyingi.
Ubunifu wa muundo wa ndani ni wa hali ya juu ambapo abiria wanapata experience ya ajabu wakiwa ndani. Sio tu muonekano wa nje unaovutia, ndani kuna vifaa vya kisasa kama vile skrini na AC zinazoweza kubadilishwa kila kiti. Hii inafanya Alphard kuwa gari ya kifahari ya kweli, inayowapa wamiliki wake hali ya kutojali umbali wa safari.
Bei Ya Toyota Alphard Tanzania
Katika soko la Tanzania, bei ya Toyota Alphard inategemea mwaka wa gari na hali yake. Kwa mfano, modeli za zamani za Alphard kama za mwaka 2002 hadi 2008 zinapatikana kati ya TSh 12,800,000 na TSh 34,000,000. lakini ukiangalia modeli mpya zaidi kama za mwaka 2021 na 2022, bei inaongezeka hadi kufika kati ya TSh 115,000,000 na TSh 165,000,000.

Car Model | Year | Price (TSh) |
---|---|
Toyota Alphard 2002 | 15,000,000 ~ 22,900,000 |
Toyota Alphard 2003 | 14,700,000 ~ 19,800,000 |
Toyota Alphard 2004 | 12,800,000 ~ 24,500,000 |
Toyota Alphard 2005 | 12,800,000 ~ 26,500,000 |
Toyota Alphard 2006 | 13,580,000 ~ 26,500,000 |
Toyota Alphard 2007 | 16,800,000 ~ 27,800,000 |
Toyota Alphard 2008 | 13,800,000 ~ 34,000,000 |
Toyota Alphard 2009 | 22,800,000 ~ 36,500,000 |
Toyota Alphard 2010 | 25,500,000 ~ 34,700,000 |
Toyota Alphard 2011 | 28,800,000 ~ 34,700,000 |
Toyota Alphard 2012 | 24,800,000 ~ 47,000,000 |
Toyota Alphard 2013 | 49,800,000 ~ 49,800,000 |
Toyota Alphard 2014 | 47,000,000 ~ 47,000,000 |
Toyota Alphard 2015 | 94,000,000 ~ 94,000,000 |
Toyota Alphard 2016 | 95,000,000 ~ 118,000,000 |
Toyota Alphard 2018 | 145,000,000 ~ 145,000,000 |
Toyota Alphard 2019 | 108,000,000 ~ 130,000,000 |
Toyota Alphard 2021 | 115,000,000 ~ 165,000,000 |
Pamoja na hizi bei kama una mpango wa kunu nua gari hii ni muhimu kuweka kwenye kumbukumbu kwamba vitu au sababu kama kodi, ushuru wa magari, na mahitaji yanaweza kuleta mabadiliko ya bei za magari haya. Viwango vya ubadilishaji wa fedha (forex) pia vinaweza kuleta mabadiliko kwenye bei, hasahasa kwa magari yanayoagizwa moja kwa moja kutoka nje ya nchi.

- BEI ZA MAGARI MENGINE:
- Bei Ya Land Rover Defender Mpya ikiwa Tanzania
- Bei ya Mazda CX-5 Mpya ikiwa Tanzania
- Bei Ya Toyota Noah Mpya ikiwa hapa Tanzania
- Bei Ya Toyota IST Mpya ikiwa hapa Tanzania
- Bei ya Lexus mpya ikiwa hapa Tanzania
- Bei Ya Toyota Hiace Used Tanzania
