Audi inamilikiwa na Volkswagen Group ilianzishwa mwaka 1909, Audi imebakia kuwa nembo imara, nembo ya ubora na utendaji. Audi ni alama ya teknolojia ya hali ya juu na gari yenye mvuto wa kipekee gari hii ni noma inamuonekano mzuri mno, Ni aina ya gari ambalo linapendwa sana na watu wenye uwezo wa hali flani nzuri, watu wenye status ndio wanapenda kumiliki gari hii ya maana kabisa.
Bei Ya Audi nchini Tanzania | Model zote
Audi gari yenye nguvu na imara ina injini bora kama vile TFSI, inayojulikana kwa kutumia nguvu bila kutumia wingi wa mafuta. Injini hizi zinafanya kazi kwa ushirikiano na teknolojia za kiusalama kama Anti-lock Braking System (ABS) na Electronic Stability Control (ESC) kulinda abiria wako au familia yako kwenye barabara.
Body ya hizi gari ni ngumu na imara imetengenrzwa kwa madinui yenye nguvu kubwa inayoweza kustahimili shida za barabarani kwa ubora wa hali ya juu. ukizingatia vitu vilivyopo ndani ya gari sasa ni vya kisasa mno na vinavutia sana muziki mzito, na AC ni ku tap tu.
Bei Ya Audi Tanzania
Makadirio ya bei za Audi Tanzania huanzia kwenye viwango tofauti kulingana na model na mwaka.

Car Model | Car Year | Engine (cc) | Price (Tsh) |
---|---|---|
Audi A3 (2010) | 2000CC | 23,000,000 ~ 26,700,000 |
Audi A4 (2005-2015) | 2000CC | 11,300,000 ~ 38,500,000 |
Audi A5 (2012-2015) | 1980CC | 37,000,000 ~ 44,900,000 |
Audi A6 (2002-2004) | – | – |
Audi A7 (2018) | – | – |
Audi Q2 (2018) | 1000CC | 61,000,000 ~ 68,000,000 |
Audi Q3 (2012-2018) | 2000CC | 33,000,000 ~ 78,000,000 |
Audi Q5 (2008-2020) | 2000CC | 32,000,000 ~ 150,000,000 |
Audi Q7 (2008-2015) | 2990CC-3600CC | 45,000,000 ~ 85,000,000 |
Audi TT (2001-2007) | 3200CC | 26,000,000 ~ 38,600,000 |
Audi Q3 (2018) | – | 78,000,000 ~ 78,000,000 |
Audi Q5 (2017/2018) | 1980cc-1990cc | 39,000,000 ~ 98,800,000 |
Audi Q2 (2018) | 1000cc, 2000cc | 60,000,000 ~ 69,000,000 |
Audi A4 2.0T Premium AWD quattro (2017) | 2000cc | 56,500,000 ~ 56,500,000 |