Toyota IST ni gari ya kawaida yenye mvuto na kubwa zaidi ni kwamba gari hii inatumia wese/mafuta kidogo sana kwa town trip, gari hii inapendwa hasa vijana wanalipenda gari hili kutokana na urahisiwake kumudu wese., nyakati hizi linapojulikana kwa majina mbalimbali duniani kama Scion xA na Scion xD huko Amerika ya Kaskazini, au Urban Cruiser katika masoko ya Ulaya na Amerika ya Kusini. IST ilizinduliwa rasmi mwaka 2002, ikilenga soko la magari madogo ya kifahari kwa vijana wenye uchangamfu na wenye kuishi mjini.
Toyota IST ina nafasi kubwa ndani, makubaliano bora kati ya ukubwa wa nje na nafasi ya ndani, pamoja na teknolojia mbalimbali zinazokidhi mahitaji ya kisasa. Inajivunia injini za 1.3L na 1.5L, na teknolojia za usalama kama airbags na teknolojia ya breki za hali ya juu. Mbali na muundo wa nje wa kuvutia, IST pia inatoa vionjo vya ndani vikiwemo vioo vya nguvu na mfumo wa urambazaji wa hiari ambao unaleta urahisi na faraja kwa dereva na abiria.
Bei Ya Toyota IST Mpya
Bei za Toyota IST mpya nchini Tanzania zinaweza kuathiriwa sana na masuala ya kiuchumi kama kodi, ushuru wa kuingiza magari na mahitaji ya soko. Kwa kawaida, bei ya IST mpya kutoka nje inaweza kuanzia TZS 14,600,000 kwa toleo la zamani hadi TZS 33,000,000 kwa toleo jipya. Bei hizi zinaweza kubadilika kutegemea na sera za kifedha na mabadiliko ya kiuchumi kama vile viwango vya ubadilishaji wa fedha.

Car Model (year) | Engine(cc) | Price (TSh) |
---|---|---|
Toyota IST (2003) | 1290 | 7,500,000 ~ 17,500,000 |
Toyota IST (2004) | 1290/1490 | 7,000,000 ~ 19,500,000 |
Toyota IST (2005 | 1290/1490 | 10,000,000 ~ 18,900,000 |
Toyota IST (2006) | 1290/1490 | 9,800,000 ~ 33,000,000 |
Toyota IST (2007) | 1290/1490 | 13,000,000 ~ 26,000,000 |
Toyota IST (2008) | 1290/1490 | 12,500,000 ~ 23,500,000 |
Toyota IST (2009) | 1490 | 14,600,000 ~ 19,500,000 |
Ukilinganisha bei za IST na magari mengine katika daraja lake utagundua kuwa IST inaweza kumudu kuwa chaguo la gharama nafuu zaidi kuliko magari mengne ya daraja lake usisahau kuhusu utumiaji wake wa mafuta ni mdogo mno na hivyo inatoa nafasi kwa watu wa kipato cha kawaida kabisa kuweza kumiliki. ukilinganisha na magari kama Honda Fit na Nissan March katika soko. Bei hizi zinaweza pia kuathirika na hata viwango vya ubadilishaji wa fedha, muenendo wa uchumi na mabadiliko katika ushuru wa kuingiza magari.
