Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kiume
Wazazi wengi wanapopata ujauzito huanza kujiuliza: Je, nitapata mtoto wa kiume au wa kike?
Kitaalamu, jinsia ya mtoto huamuliwa mara tu mbegu za kiume (sperms) zinapokutana na yai, kulingana na kromosomu zilizobebwa (X au Y). Hata hivyo, hadi sasa hakuna dalili za mwili zinazoweza kuthibitisha kwa uhakika jinsia ya mtoto bila vipimo maalumu.
Hata hivyo, kwa muda mrefu, jamii mbalimbali zimekuwa zikihusisha baadhi ya dalili za ujauzito na kupata mtoto wa kiume. Dalili hizi si za kisayansi 100%, bali ni imani na uzoefu wa baadhi ya wanawake.
Dalili Zilizohusishwa na Mimba ya Mtoto wa Kiume
1. Tumbo Kusogea Chini
Inasadikika kuwa mama mjamzito mwenye mtoto wa kiume mara nyingi hubeba mimba chini ya kitovu, tofauti na mtoto wa kike ambapo tumbo huonekana juu zaidi.
2. Kukosa Kichefuchefu Kingi
Wengine huamini mimba ya kiume huleta kichefuchefu kidogo zaidi, ukilinganisha na mimba ya kike.
3. Hamu ya Chakula Chenye Chumvi na Protini
Wanawake wajawazito wa watoto wa kiume mara nyingi hujisikia kutamani nyama, chips, samaki, mayai au vyakula vyenye chumvi zaidi.
4. Ngozi Kuwa Safi
Inavyodaiwa, mtoto wa kiume “hampoki uzuri” mama, hivyo ngozi hubaki safi na yenye kung’aa zaidi.
5. Mapigo ya Moyo ya Mtoto Kuwa Chini
Kitaalamu, mapigo ya moyo ya mtoto huchukuliwa kwenye ultrasound. Kuna imani kuwa mapigo chini ya 140 bpm huashiria mtoto wa kiume (ingawa sayansi haijathibitisha moja kwa moja).
6. Nywele Kuwa Nene na Kung’aa
Baadhi ya wanawake husema nywele zao zinakuwa nzuri, nene na zenye afya zaidi wanapokuwa na mimba ya mtoto wa kiume.
7. Kutokuwa na Mabadiliko Makubwa ya Hisia
Wengine huamini mimba ya mtoto wa kiume haileti “mood swings” makali kama ilivyo kwa mtoto wa kike.
8. Miguu Kuwa Baridi
Kuna imani kuwa miguu baridi mara kwa mara ni dalili ya kuzaa mtoto wa kiume.
9. Kupenda Kukaa au Kulala Ubavu wa Kushoto
Baadhi ya wanawake husema wanahisi raha zaidi kulala upande wa kushoto wanapobeba mimba ya mtoto wa kiume.
10. Kuongezeka kwa Njaa
Inasemekana kuwa mama hubeba mimba ya kiume anapokuwa na hamu ya kula mara kwa mara na kwa wingi.
Vipimo vya Kisayansi vya Kujua Jinsia
Kwa uhakika, njia pekee ya kujua jinsia ya mtoto ni kwa kutumia vipimo vya kitabibu:
- Ultrasound (kuanzia wiki ya 16–20 ya ujauzito).
- Amniocentesis na Chorionic Villus Sampling (CVS) (kwa ajili ya kuchunguza afya ya kijusi, lakini pia hufichua jinsia).
👉 Kwa maelezo ya vipimo vya mimba na jinsi ya kujua muda wa kujifungua, soma hapa: Kipimo cha ujauzito na muda wa kujifungua.
Hitimisho
Dalili kama tumbo kubebwa chini, hamu ya vyakula vyenye chumvi, ngozi kuwa safi, na kichefuchefu kidogo huaminika kuashiria mimba ya mtoto wa kiume. Hata hivyo, dalili hizi si za uhakika na hutofautiana kati ya mama mmoja na mwingine. Njia pekee ya kuthibitisha jinsia ni kupitia vipimo vya kitabibu.
Chanzo cha taarifa za afya: Medical Stores Department – MSD