Dalili za yai kupevuka kwa mwanamke msichana au binti
Mwili wa mwanamke unatoa mabadiliko ya aina mbalimbali kuonesha kwamba hizi ni siku za hatari na yai limekuwa tayari kurutubishwa Kwa baadhi ya wanawake itakua tofauti, lakini kuna dalili mama zile ambazo almost wanawake wengii sana wanazipitia pindi yai linapokuwa limeshapevuka tayari kwa kurutubishwa Chini ni dalili kubwa zaidi zinazoashiria kwamba yai limekomaa na hivyo mwanamke awe na tahadhari au acheze kwa tahadhari kubwa wakati wowote akirutubishwa tu mimba inatungwa.
1.Kuvuja Uteute
Lazima utakuwa umewahi kusikia kuhusu ute wa uzazi ama ute wa ovulation, ama kuona uchafu mwembemba unaovutika kwenye chupi. Huu ndio ute unaoashiria kwamba yai limepevuka na litatolewa ndani ya masaa 24 tangu ute umeanza kutoka. Uteute huu unakuwa mwepesi kama yai, unavutika na hauna harufu. ukiona dalili hii ya uteute jua kua tayari chakula kimeiva.
Soma pia: Njia rahisi za kumfikisha mpenzi wako kileleni
2.Tumbo linasumbua
Hii inatokea wakati ambao huna ugonjwa wowote ule lakini unashangaa tumbo linajaa gesi Mabadiliko ya homoni hasa kuongezeka kwa homoni (Luteinizing hormone (LH) la LH inaweza kufanya tumbo kubaki na maji na hivo litakua limejaa kiasi fulani. hali hii inatokeaga kwa muda kidogo kisha unakua sawa kabisa hii ina maanisha upo tayari kuijaza dunia endapo utarutubishwa vizuri.
Pia soma: Jinsi ya kumvutia Msichana na Kumfanya Akutamani kimapenzi
3.Hali ya Kichefuchefu
Zinapokaribia siku za yai kupevuka siku 2 kabla huwa kuna hali ya kichefuchefu cha mara kwa mara hii huwa inaenda hadi siku husika ambayo yai litakua linapevuka Unaweza kupata hali ya kuhisi kichefuchefu ukiwa kwenye siku ya ovulation, hii pia ni kutokana tu na mabadiliko ya homoni. Endapo utapata na hali hii, jaribu kutembea nje upate hewa safi lakini jua kwamba mambo yameiva.
Soma pia: Hizi hapa dalili za kukojoa kwa mwanamke mkiwa kwenye tendo.
4.Mabadiliko ya joto la mwili
Hii ni hali ya kimwili ambayo inatokea na muhusika mwenyewe ndio anaweza kluhisi hali isiyokuwa ya kawaida na kwamba joto limepanda Kwenye siku za hatari, hasa siku yenyewe yai linapotolewa, joto la mwili huongezeka kidogo kwa centigrade kadhaa kama 0.3. Unaweza kununua kipimajoto pharmacy ukajipima mwenyewe nyumbani na kuona mbadiliko haya.

5.Maumivu ya tumbo
Unaweza kupata maumivu kipindi cha yai kutolewa, Maumivu haya yanatokana na kitendo cha yai kutoka kwenye kikonyo chake ambacho ni mfumo wa mayai(ovari). Kitendo hiki pia chaweza kupelekea damu itoke kwenywe kovu na hivo ukaona matone kidogo kwenye chupi. Kuanzia sasa endapo utaona damu kidogo katikati ya mzunguko basi usiogope, jua tu ni mfumo wa ovari.
Pia Soma: Mambo ya kuzingatia unapokuwa na mpenzi wako Usiku wa Kwanza
Hitimisho
Kama unataka kujua kwamba wewe na mwenzi wako mfanye tendo lini ili kuongeza nafasi ya kupata mimba haraka Siku nzuri na yenye nafasi nzuri kutunga mimba ni siku 5 kabla ya yai kutolewa na siku ambapo yai limetolewa hadi masaa 24 yanayofuata.
Kwanini siku 5 kabla? kwasababu mbegu zinaweza kuishi mpaka siku 5 kwenye kizazi baada ya kufanya mapenzi (tendo). hasa mbegu za kiume zina uwezo wa kusubiri na yai likitoka tu linarutubishwa barabara.
Kila mwanamke azingatie mfumo wake wa mzunguko kwa sababu kila mwanamke ana mfumo wake tofauti na mwengine.
