Dhahabu nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa sana hupatikana katika ukanda wa Ziwa Victoria, Mikoa iliyopo karibu na na ziwa victoria lakini hasahasa maeneo haya yafuatayo eneo la Lupa Gold Field, Mpanda Mineral Field, na ukanda wa dhahabu wa Tanzania Mashariki.
Kanda ya Ziwa Victoria
Eneo hili lina migodi mikubwa ya dhahabu kama Bulyanhulu, Geita (inayomilikiwa na AngloGold Ashanti), Buzwagi, na North Mara (inayomilikiwa na Twiga Minerals Corporation, ubia kati ya Barrick Gold Corporation na Serikali ya Tanzania).
Lupa Gold Field
PROJECT hii ya uzalishaji wa dhahabu ni sehemu ya mgodi wa dhahabu wa New Luika (unaomilikiwa na Shanta Gold) katika Wilaya ya Songwe.
Mpanda Mineral Field
Mkoa huu pia unajulikana kwa kuwa dhahabu hasa kwa sababu ya uwepo wa migodi mingi midogo midogo lakini pia kuna project kubwa za dhahabu na tayari serikali ya tanzania imeshasaini mikataba ya utekelezaji wa kuanza kazi za uchenjuaji wa dhahabu pale Mpanda.
Soma na hii: Bei ya Dhahabu hii leo tanzania
Mgodi wa Dhahabu wa Geita
Sasa huu ndio mkoa maarufu zaidi kwa upatikanaji na uchimbwaji wa madini ya dhahabu mkoa huu unapatikana kaskazini-magharibi mwa Tanzania, karibu na Mwanza, vyanzo vya madini hayo inasadikika ni kutoka kwenye shimo la wazi la Nyankanga na migodi miwili ya chini ya ardhi (Star na Comet pamoja na Nyankanga).
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara
Mgodi huu unasifika kwa uwezo wake wa kuzalisha dhahabu safi na nyiongi mgodi unapatikana katika wilaya ya Tarime mkoani Mara, karibu kilomita 100 mashariki mwa Ziwa Victoria na 20km kusini mwa mpaka wa Kenya.
New Luika Gold Mine
Mgodi huu unajulikana kwa kazi yake ya kuzalisha dhahabu bora na mgodi umekuwepo nchini zaidi ya miaka 30 hivyo umechangia pato la taifa kwa kiasikikubwa mgodi huu unapatikana katika Wilaya ya Songwe, Kusini-Magharibi mwa Tanzania, takriban kilomita 700 kusini-magharibi mwa Dar es Salaam
Hitimisho
Kama wewe ni mfanyabiashara aua unataka kufanya biashara ya dhahabu unatakiwa kuwa updated kuhusiana na wapi Dhahabu inapatikana kwa wingi nchini tanzania, Soko la dhahabu ni mojawapo ya masoko yenye high volatility nchini kwetu tanzania, Mabadiliko haya ya bei kila mara yanasababishwa na masoko makubwa ya kudunia au nguvu za uhitaji na upatikanaji wa dhahabu yenyewe nchini.