FAQ
Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)
A: Ajira Serikalini
1. Jinsi gani ninaweza kutuma maombi ya kazi serikalini?
Tembelea portal ya ajira, unda akaunti, jaza taarifa zako, na omba nafasi za kazi moja kwa moja kupitia mfumo huo.
2. Je, ni lazima kuweka barua ya maombi?
Ndiyo. Barua ya maombi ni nyaraka muhimu ya kuonyesha dhamira na sababu zako za kutaka kazi hiyo.
3. Nyaraka gani zinahitajika kuambatanishwa?
CV, barua ya maombi, vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa, na taaluma nyingine kama inahitajika.
4. Nafasi za kazi hupatikana wapi rasmi?
Ajira zote serikalini hupatikana kupitia Ajira Portal.
5. Nitawezaje kufuatilia status ya maombi yangu?
Ingia akaunti yako kwenye Ajira Portal, nenda sehemu ya “My Application” kuona maendeleo ya maombi yako.
Jinsi ya Kuandaa CV
1. Ni vitu gani lazima viwe kwenye CV?
Jina lako, mawasiliano, elimu, uzoefu wa kazi, ujuzi, lugha unazozungumza na referees.
2. CV inapaswa kuwa na kurasa ngapi?
Kurasa 1 hadi 2 zinatosha, ila muhimu ni kuweka taarifa muhimu tu.
3. Je, ni sawa kutumia template kutoka mtandaoni?
Ndiyo, lakini hakikisha unazibadilisha ili ziendane na nafasi ya kazi unayoomba.
4. Picha kwenye CV ni lazima?
Si lazima, lakini inaweza kuwa na faida kwa baadhi ya kazi kama huduma kwa wateja au uwakilishi.
5. Jinsi ya kufanya CV iwe ya kuvutia zaidi?
Weka vichwa vidogo vizuri, tumia lugha rasmi, na onyesha mafanikio yako kwa vielelezo au takwimu.
Elimu
1. Jinsi gani naweza kujiunga na chuo kikuu Tanzania?
Tembelea TCU au chuo husika, fuata maelekezo ya udahili na jaza fomu ya maombi mtandaoni.
2. Je, kuna mikopo ya wanafunzi vyuo vikuu?
Ndiyo. Mikopo hutolewa na HESLB. Unatakiwa kutuma maombi kupitia mfumo wao wa mtandao.
3. Vyeti vilivyopotea vinaweza kurudishwa vipi?
Toa taarifa ya kupotea polisi, kisha nenda baraza husika la mitihani kuomba nakala mpya.
4. Je, naweza kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili?
Ndiyo, zipo scholarships nyingi – unaweza kutafuta kupitia websites kama DAAD, Chevening, au HESLB.
5. Kuna tofauti gani kati ya diploma na certificate?
Certificate ni stashahada ya awali, na diploma ni ngazi ya juu zaidi – mara nyingi miaka miwili au mitatu.
Biashara
1. Biashara gani inalipa zaidi Tanzania?
Biashara za vyakula, usafirishaji, urembo, simu, na kilimo cha kisasa ndizo zinalipa zaidi kwa sasa.
2. Nawezaje kuanzisha biashara bila mtaji mkubwa?
Anza na ujuzi ulionao, tumia mitandao ya kijamii kuuza bidhaa au huduma, au fanya dropshipping.
3. Je, natakiwa kusajili biashara yangu?
Ndiyo. Tembelea BRELA kwa usajili rasmi wa jina la biashara, TIN number, na leseni ya biashara.
4. Biashara ya mtandaoni ni halali Tanzania?
Ndiyo, mradi ufuate sheria za kodi, usajili, na utoe huduma halali kwa wateja wako.
5. Nawezaje kupata mkopo kwa ajili ya biashara?
Unaweza kuomba mikopo kupitia SACCOS, benki kama NMB, CRDB, TPB au taasisi kama SELF Microfinance.