Nafasi za Kazi AzamPesa: Head of Sales & Senior Revenue Assurance Analyst (September 2025)
Kampuni ya AzamPesa inatangaza nafasi mbili muhimu kwa ajili ya wataalamu wenye weledi na ari ya kufanya kazi kwa ubunifu. Hizi nafasi ni:
- Head of Sales (Mkuu wa Mauzo)
- Senior Revenue Assurance Analyst (Mchambuzi Mwandamizi wa Mapato)
Mwisho wa kutuma maombi: 10 Oktoba 2025
1. Head of Sales (Mkuu wa Mauzo)
Maelezo ya Kazi
Mkuu wa Mauzo atakuwa kiongozi mwenye uwezo wa kuuza bidhaa za AzamPesa, kusimamia rasilimali na kuhakikisha mikakati ya kampuni inatekelezwa ipasavyo. Atahitaji ubunifu katika kuelewa soko, kurekebisha mbinu kulingana na matokeo na mrejesho, pamoja na kubaini mianya ya kibiashara katika sekta ya fedha za simu ili kuandaa mbinu zinazopenya masoko hayo.
Majukumu haya pia yanahusisha kuanzisha na kudumisha utamaduni wa uadilifu, uaminifu na ubora katika shughuli zote za mauzo.
Sifa za Mwombaji
- Shahada ya Biashara, Fedha au fani inayohusiana (au sawa na hiyo).
- Uanachama katika taasisi au vyama vya kitaaluma vinavyohusiana.
- Vyeti au uthibitisho wa kitaaluma katika maeneo husika.
- Angalau uzoefu wa miaka 5 katika mauzo na masoko kutoka sekta yoyote.
- Mtazamo wa mteja kwanza na mbunifu wa suluhisho.
Majukumu Makuu
- Kusimamia rasilimali na kuhakikisha mauzo yanaendana na mkakati wa kampuni.
- Kuhakikisha wateja wapya (binafsi na makampuni) wanaleta tija kwa kampuni.
- Kuboresha na kuendeleza njia za usambazaji.
- Kukuza ujuzi wa timu na kuhakikisha elimu inahamishwa.
- Kufanikisha malengo ya mauzo na usambazaji wa huduma za AzamPesa.
- Kuongoza timu ya mauzo ya moja kwa moja kufikia malengo kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
- Kufanya mapitio ya utendaji wa mauzo kila mwezi kwa kanda na maeneo yote.
- Kufuatilia mrejesho wa bidhaa na shughuli za washindani.
- Kuandaa na kusimamia kampeni na promosheni kwa kushirikiana na wadau husika.
- Kudumisha uelewa wa kina wa washindani na mwenendo wa soko.
Maarifa na Ujuzi
- Uelewa mpana wa kujenga na kusimamia mtandao wa mauzo Tanzania.
- Ujuzi bora wa mawasiliano, uwasilishaji na mazungumzo.
- Uwezo wa kuchambua na kuandaa taarifa kwa usahihi.
- Ujuzi wa Microsoft Office.
- Uadilifu wa hali ya juu na tabia ya kuaminika.
2. Senior Revenue Assurance Analyst (Mchambuzi Mwandamizi wa Mapato)
Maelezo ya Kazi
Mchambuzi Mwandamizi wa Mapato atasimamia ukaguzi wa kina wa mikondo ya mapato, kuhakikisha usahihi na uadilifu wa data za kifedha na miamala. Atakuwa mstari wa mbele kugundua mianya ya mapato, visa vya udanganyifu na kuweka mifumo ya kudhibiti upotevu wa mapato kwa kutumia teknolojia za kisasa (AML/AI na zana za uchambuzi wa data).
Sifa za Mwombaji
- Shahada ya Biashara, Fedha au fani inayohusiana (au sawa na hiyo).
- Uanachama katika taasisi au vyama vya kitaaluma vinavyohusiana.
- Vyeti au uthibitisho wa kitaaluma katika maeneo husika.
- Angalau uzoefu wa miaka 5 katika revenue assurance, ukaguzi wa ndani, usimamizi wa fedha au udhibiti wa hatari.
- Uzoefu wa angalau miaka 3 katika nafasi ya juu kwenye taasisi yenye miamala mingi (mfano: benki, fintech, telecom, malipo).
Majukumu Makuu
- Kufuatilia na kuthibitisha data za kifedha na miamala kila siku.
- Kuchunguza viashiria vya udanganyifu vilivyotolewa na mifumo ya AML/AI na kuchukua hatua stahiki.
- Kubaini chanzo cha upotevu wa mapato, kupendekeza suluhisho na kufuatilia utekelezaji wake.
- Kutengeneza na kuweka mifumo ya kudhibiti udanganyifu na kupunguza hasara.
- Kuandaa na kuwasilisha ripoti za mapato kila siku, wiki na mwezi kwa uongozi.
- Kushirikiana na timu za Fedha, IT, Uendeshaji na Uzingatiaji Sheria kuhakikisha usalama wa mapato.
- Kufundisha na kusimamia wachambuzi chipukizi ndani ya timu.
- Kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka zote za ukaguzi na uchunguzi.
Maarifa na Ujuzi
- Uelewa wa mifumo ya bili na ERP (SAP/Oracle/Sage).
- Uzoefu wa kutumia zana za Business Intelligence (Power BI, Tableau).
- Uelewa wa viwango vya uhasibu (IFRS/GAAP).
- Ujuzi wa uchambuzi, udhibiti wa data na usimamizi wa miradi.
- Tabia ya uadilifu, uwajibikaji na uongozi bora.
Namna ya Kutuma Maombi
Wataalamu wenye sifa waliotayari kuchangia katika ukuaji wa huduma za kifedha za kidigitali wanaalikwa kutuma maombi yao kwa nafasi husika:
Mwisho wa kutuma maombi: 10 Oktoba 202
Jiunge na community yetu — Shiriki, Jifunze, Changia
Ungana na wanachama wengine wa Wikihii, ulizoni maswali, toa maarifa, pata taarifa za ajira, na upokee updates za kipekee kutoka kwa mtaalam wetu.
