BIASHARA YA FOREX PDF
Karibu sana kwenye hii makala ambapo nimeamua kuandika mambo kadhaa ya kuweka kwenye kumbukumbu zako kama una ndoto au nia ya kuwa forex trader, Makala hii itakusaidia kuelewa mambo ya msingi yanayolizunguka soko la forex na nini cha kufanya kwa mazingira mbalimbali. Kwa uzoefu wangu nimekutana na watu wengi sana wenye passion ya kuwa traders na kuendesha maisha kupitia trading, believe me ni nusu tu ya watu wote niliowafahamu na kuwashauri ndio wamefanikiwa kiasi Fulani. Hii ni situation ambayo haielezeki, Katika tasnia nyingi sana iwe ujenzi wa nyumba, ufundi wowote ule, au kilimo ama hata ufugaji tasnia zote hizo na nyinginezo ukijifunza kwa juhudi na maarifa basi kuna uwezekano mkubwa ukatoboa kupitia hiyo tasnia, Lakini hiyo SIO kweli kwenye Tasnia ya FOREX TRADING, Na hapo ndipo kunaitofautisha Forex na tasnia nyingine zote.
FOREX NI MTEGO
Hata siku moja usiichukulie FOREX sawasawa na Tasnia nyingine ukiwa na hilo wazo basi tayari hicho ni kikwazo kuelekea kwenye forex, Kwenye trading ni uwanja mwingine kabisa tofauti na viwanja vingine, Trading ina namna yake ya kufanya na utaratibu wake wa kipekee kabisa ambao kuwezi kuukuta kwenye tasnia (industry) nyingine. Kwenye trading ni sehemu ambayo unawekeza PESA AKILI NA HISIA ZAKO.
Kwenye forex unawekeza pesa, akili na hisia vyote hivi kwa wakati mmoja na hapo ndipo MTEGO WENYEWE ULIPO, sehemu ambayo unaweka pesa, akili na hisia kwa wakati mmoja ni BINADAMU wachache sana wenye uwezo wa kuwa na consistent hasa ukizingatia kwamba unaweka pesa ili upate pesa lkn sokoni ku nakua na matokeo mawili either upate au upoteze.
Na ndio maana kuna wataalamu wengi kwenye tasnia mbalimbali ambao walijaribu kuja kwenye trading wakiamini kwamba wao ni smart sana na kwmba wanaweza kufanikiwa kirahisi llakini takwimu zinasema kwamba watu wa namna hiyo ndio wanaongoza kwa kufeli sana wanapokuja kwenye trading. Kwa sababu Forex ni uwanja tofauti na viwanja vyote ulivyowahi kucheza.
Unaweza kuwa na PESA ukafelishwa na HISIA, na unaweza kuwa na AKILI ukafelishwa na HISIA na viceversa, HISIA (FEELINGS) Zina maana pana ssana tukiwa kwenye upande wa trading usizichukulie poa hata kidogo yani kwa taarifa tu ni kwamba kwenye trading kuna concept inaitwa TRADING PSYCHOLOGY Hii trading psychology ndio HISIA ZAKO UNAZOWEKEZA KWENYE FOREX MARKET. Hii ndio mchawi wa watu wote wanaoingia kwenye forex wakiamini kwmba wao ni smart sana kuliko wengine.
Hapa nataka niweke story kidogo kwenye maisha utakua ushakutana na watu amabao hawana elimu wanaonekana ni washamba na pengine wapo kijijini lakini unakuta mtu anamiliki nyumba nyingi, mashamba mengi, na hata semitrella kadhaa, mm kwakua nimekulia vijijini nimewaona sana watu ambao wameishia darasa la saba 7 lakini mwisho wa siku ndio watu ambao wana mafanikio kwenye jamii. Nikawa nina swali kwamba kwanini wasomi wengi kwenye jamii wanashindwa kufanikiwa kabisa ktk haya maisha.
Taratibu nikaanza kuelewa kwamba mtu mwenye akili / elimu ana kiburi cha kuamini kwamba yeye anastahili vitu bora, na mtu asiye na elimu hana cha kupoteza hii ni tofauti kati ya wasomi wengi sana na washkaji wasiokuwa na elimu mtaani.
Kwenye forex kuna fomula nyingi, tactics nyingi, strategies nying sana na strategy zote zinafanya kazi some time na hazitofanya kazi some time kwenye mazingira Fulani yakibadilika, USIKARIRI kwa sababu forex sio kama kujenga nyumba kila siku utajenga kwa fomula ileile kwenye forex fomula inabadilika kila wakati kulingana na conditions mbalimbali zinazotokea sokoni. Na hii ni kweli almost kwenye tasnia nyingi sana kwamba ukishafahamu kitu Fulani basi umejua kila siku utatumia mfumo uleule kufanya kazi, Lakini hiyo siyo kweli kwenye forex trading.
FOREX NI VITA
Ukiisikia forex siku za mwanzo unaweza kuzani kwamba ni njia rahisi sana kutengeneza pesa, na unaweza kusoma kidogo ukajiona tayari unatosha kwenda kuchuma pesa kwenye masoko ya forex, amini kwamba hii mentality kila trader anayeanza biashara au aliyeisikia forex hivi karibuni na akaanza kuifuatilia / kuifanya huwa anaamini hivyo kwamba forex ni rahisi na anaweza kuendesha maisha kwa forex kirahisi, Hii ilinitokea mimi wakati naanza forex HADI nilipokuja kusoma deep kuhusu forex na nilipoelewa hasa soko la forex linavyofanya kazi hapo ndipo niliagundua kwamba FOREX NI VITA KUBWA SANA na kwamba mtu akiingia vitani bila maandalizi lazima atapoteza vita, sharia hii ni muhimu sana kuizingatia mapema sana kwa sababu wahusika wakubwa kwenye trading ni mabenki, taasisi kubwa za kifedha, hedge funds, serikali kupitia benki kuu (central bank) halafu kuna mimi na wewe (retail traders) kwahiyo mara zote unapotrade maana yake unatrade pamoja au sawasawa na hao wahusika wengine (hedge funds, banks, Institution traders) wenye akili kubwa maarifa mengi na uzoefu wa kutosha kwenye hii kazi na kila mhusika anatambua jinsi ya kutengeneza faida dhidi ya mwenzake na hapo ndipo forex inapogeuka kuwa uwanja wa VITA.
Ili kuibuka mshindi kwenye vita ya forex ni muhimu kutulia kutuliza akili na kuelewa mambo ya msingi ikiwa ni pamoja na ukweli usiofichika kwamba soko la forex litakuwa unique wakati wote, kuna wakati utapoteza, na siku zote utabaki kuwa mwanafunzi wa masoko, nilifanikiwa kwenye forex trading baada ya kuelewa na kuyakubali haya mambo matatu.
Haya mambo matatu ukiyaelewa na kuyakubali kwamba ndio ukweli uliopo kwenye forex basi yatakusaidia sana kujua nini kinaendelea sokoni na ni jinsi gani uyachukulie matokeo yoyote yatakayopatikana kwenye vita na jinsi ya kujidhibiti wewe mwenyewe kwenye trading na kwa namna gani uichukulie trading hivi vitu vyote vinakua muhimu sana kwa sababu soko halina mazoea sio kama ng’ombe wa maziwa kwamba kila siku utamkamua maziwa hii kwenye trading sio kweli kuna siku zitatokea ng’ombe hatatoa maziwa au atatoa maziwa kidogo, au atatoa maziwa mengi kuzidi huu ndio ukweli wa forex trading kinsingi kufanya trading ni kuishi kwa imani haya mambo yote trader anatakiwa kuyabalance na kuishi nayo siku zote za career yake, unaweza kusema forex ina utaratibu tofauti wa maisha mtu anatakiwa awe na akili flani au mitazamo flani tofauti na watu wengi ili aweze kufanikiwa kwenye hii kazi, ndio maana watu wachache waliofanikiwa kwenye trading huwa wanakuwa smart sana kichwani hata kwenye mambo mengine ya kimaisha ya kawaida ukiacha biashara ‘
Kitu kizuri ni kwamba haikuhitaji uwe na elimu kubwa, kupata mafanikio kwenye trading, Hata ukiwa na elimu ya darasa la saba ukiwa tayari kufuata utaratibu, kuzingatia na ukipata mwalimu sahihi kuna uwezekano mkubwa ukawa trader na ukapata mafanikio ya muda mrefu kwa sababu ya kufuata utaratibu kuheshimu sharia za game na siku zote kuwa mwanafunzi msikivu wa masoko hata kama unatengeneza faida.
Kama ambavyo kwenye maisha yetu tunavyoona kuna watu wengi hawana elimu na wamefanikiwa sana kwa sababu tu wamekuwa wasikivu wanafuata sharia za game na kila siku wanajiongeza na kukubali kujifunza,
FIKIRIA NJE YA BOX
Forex traders wengi wanapoanza biashara huwa wanafikiria kuhusu mbinu gani watatumia itawapa matokeo mazuri ya faida wengi wanatafuta either technical strategies wachache fundamental strategies kwa experience ya Tanzania lkn swali moja tujiulize kungekuwa na hiyo mbinu maana yake ingekua rahisi sana kutengeneza pesa na kwamba watu wengi wangekuwa nayo wangekua wanaprint pesa kila muda lkn kwnn hakuna hicho?, Jibu ni kwamba hakuna njia moja yenye muendelezo wa matokeo chanya na vice versa, lkn hata ukiamua kujua mbinu nyingi bado haitakusaidia kwa sababu kuna maelfu ya mbinu zipo nyingi sana na zote zinapewa promo kiasi kila mbinu mpya unayokutana nayo unadhani ni bora kuliko mbinu yako ya mwanzo na hii inatengeneza tabia ya kuwa kila siku unatafuta mbinu unaacha kufuatilia mambo ya msingi kama tulivyoyajadili kwenye paragraph ya juu (Forex ni Vita).
Ni kweli kwenye forex tunatrade kwa kutumia mbinu mbalimbali lakini elewa kwamba mbinu peke yake haziwezi kukupa mafanikio kwenye forex, najua utakua unajiuliza sasa kama sio mbinu nini kinachofanya mtu afanikiwe kwenye trading?
Mbinu zote zina matokeo chanya wakati Fulani na zinakua na matokeo hasi wakati Fulani hivyo kwa hii fact hatuwezi kuziamini mbinu pekee halafu tukategemea kwamba tutatoboa kwenye trading kupitia mbinu ziwe technical ama fundamental zote hazina uhakika wa 100%
Kinachomtofautisha trader aliyefanikiwa na trader asiyefanikiwa ni uwezo wa kutumia mbinu sahihi katika mazingira sahihi, na uwezo wa kuweza kuendana na mazingira ya soko kila yanapokuwa yanabadilika kutokana na forces za demand na supply.