Jinsi ya Kujaza Green Card Lottery
Mwongozo wa Uhamiaji • DV Lottery
Maneno Muhimu: Green Card Lottery, DV Program, jinsi ya kujaza DV, Entrant Status Check, DS-260, Visa Bulletin, picha ya DV.
Green Card Lottery (DV Program) ni nini?
Diversity Visa (DV) Program ni bahati nasibu ya Serikali ya Marekani inayotoa idadi maalum ya green card kila mwaka kwa watu wanaotoka nchi zenye uhamiaji mdogo kuelekea Marekani. Uchaguzi ni wa nasibu miongoni mwa walioomba na waliokidhi vigezo vilivyowekwa. Ukishachaguliwa (Selected), utaendelea na hatua za DS-260, uchunguzi wa afya, na mahojiano ya ubalozini kulingana na Visa Bulletin.
Masharti ya Kuomba Green Card
- Nchi ya Kuzaliwa: Kwa kawaida ustahiki hutegemea nchi ya kuzaliwa (si uraia). Nchi zingine hubadilika kila mwaka kulingana na viwango vya uhamiaji.
- Elimu/Uzoefu: Angalau Kidato cha Nne au uzoefu wa miaka 2 katika kazi inayohitaji mafunzo maalum ndani ya kipindi kinachotajwa.
- Picha Sahihi ya DV: Picha ya hivi karibuni, uso ukiwa wazi, background plain, bila kofia/miwani ya giza; mwelekeo wa uso mbele.
- Ukweli wa Taarifa: Majina, tarehe ya kuzaliwa, ndoa/Watoto lazima vilingane na nyaraka zako halisi (pasipoti, vyeti).
- Duplicate entries: Usitume maombi mawili kwa mtu mmoja ndani ya mwaka huo—husababisha disqualification.
- Picha isiyokidhi vigezo: Vichujio, background yenye michoro/rangi isiyo sahihi, au picha ya zamani mno.
Hatua za Kuomba Green Card (Kujaza Fomu)
1) Andaa Kwanza (Checklist Kabla ya Kujaza)
- Pasipoti halali (majina yaandikwe kama yalivyo kwenye pasipoti).
- Picha ya DV iliyoandaliwa kulingana na mahitaji (ukubwa/uwiano/sura mbele).
- Taarifa za ndoa (cheti cha ndoa/talaka) na orodha ya watoto wote wanaostahili (pamoja na picha zao sahihi).
- Anwani sahihi ya barua pepe na anwani ya posta (Mailing Address).
2) Kujaza Fomu Hatua kwa Hatua
- Taarifa Binafsi: Andika majina (Family/Last, Given/First, Middle) kwa mpangilio sahihi, jinsia, tarehe na nchi ya kuzaliwa.
- Nchi ya Ustahiki: Kwa kawaida ni nchi ya kuzaliwa (si lazima uraia). Kuna kanuni maalum kwa mwenza/wazazi katika hali fulani.
- Pakia Picha ya Mwombaji: Tumia picha mpya isiyo na vichujio, uso mbele, background plain, bila kofia/miwani ya giza.
- Anwani ya Posta: Jaza mtaa/sanduku la posta, mji, mkoa, nchi—kwa mawasiliano yanapohitajika.
- Mahali Unapoishi Sasa: Chagua nchi uliyo nayo makazi kwa sasa.
- Namba ya Simu na Barua Pepe: Tumia barua pepe inayofanya kazi—itasaidia pia kurudisha confirmation ikipotea.
- Elimu, Hali ya Ndoa, na Watoto: Chagua kiwango chako cha elimu, weka hali ya ndoa ya sasa, kisha orodhesha watoto wote wanaostahili; hakikisha picha zao pia zipo sahihi.
- Ukaguzi wa Mwisho: Hakiki majina/tarehe/adresi kabla ya kutuma (Submit).
- Hifadhi Confirmation Number: Pakua kama PDF, chukua screenshot, na jitumie barua pepe ili isipopotee.
3) Baada ya Kutuma
- Entrant Status Check: Tumia Confirmation Number kukagua matokeo pindi yanapotangazwa.
- Ukichaguliwa: Jaza DS-260, kusanya nyaraka (vyeti vya kuzaliwa/elimu, police clearance, vyeti vya ndoa/talaka, pasipoti), fanya medicals hospitali iliyoidhinishwa, kisha subiri mwaliko wa mahojiano kulingana na Case Number yako kuwa current kwenye Visa Bulletin.
Viungo vya Ndani Unavyoweza Kupenda
- Forex Tools & Resources — rasilimali muhimu za fedha unazoweza kuzitumia unapopanga mipango ya uhamiaji/safari.
- Kalenda ya Uchumi (Forex) — kufuatilia matukio ya kiuchumi duniani.
Jiunge na MPG Forex kwenye WhatsApp kwa vidokezo na masasisho