Kuendesha magari unatakiwa kuwa na leseni iliyo HAI, Leseni kwa kawaida huwa ina expire/kuisha muda wake wa matumizi kila baada ya miaka mitano (5). madereva wote magari makubwa kwa madogo wanatakiwa kufuata huu utaratibu wa kurenew leseni pindi zinapokuwa zimeisha muda wa matumizi barabarani
Kwenye hii article tunajadili utaratibu unaotumika kurenew leseni za udereva kwa madereva wote magari makubwa kwa madogo,
Vitu muhimu katika kurenew leseni
Kurenew leseni kubna vitu muhimu ambavyo unatakiwa kuwa navyo Ili ukienda TRA kurenewe usi[pate usumbufu kuhusu documents za muhimu zinazohitajika.
- Kitambulisho Cha Taifa
- Picha za pasport za wakati huo
- Leseni ya udereva (Iliyokwisha)
- Baada ya kukamilisha vifaa hivi hatua inayofuata ni kutembelea Ofisi za TRA
Tembelea ofisi za TRA tanzania Mkoa wowote ukiwa na documents zote kama tulivyoainisha hapo juu
Ukifika TRA na documents zote muhimu basi kuna Fomu watakupa uijaze, Lkn pia hii Fomu unaweza kuipata Mtandaoni (ukadownload) na kwenyewe pia ukidownload unajaza kisha unaenda kwenye ofisi ya TRA karibu na wewe ukiwa na Fomu yako uliyopakua online ukaijaza kisha unakuwa na viambatanisho muhimu kama tulivyoainisha paragraph ya kwanza.
Gharama za ku renew Leseni
Gharama (TZS) | Muda wa kuishi leseni |
---|---|
Tsh 70,000 | Miaka mitano (5) |
Ukimaliza mchakato wa kuwasilisha fomu pamoja na viambatanisho au documents zako hakikisha umelipia pesa taslim kwenye account ya serikali ambayo utaiona kwenye fomu yako, SASA hapo utapewa risiti na utapangiwa tarehe amabyo kitambulisho chako kipya kitakuwa tayari.