Jinsi ya kufungua youtube channel na utaratibu wa kulipwa
Online ni sehemu ambayo unaweza kutengeneza pesa bila mtaji! Yes, kinachotakiwa ni smartphone yako nzuri na Access ya internet bundle kwenye maishaa yako ya kila siku, moja kati ya mchongo ambao haukuhitaji uwe na mtaji ili kuianzisha online ni huu mchongo wa Youtube channel, mtu yeyote anaweza kumiliki account ya youtube kwahiyo kila mtu anaweza kumiliki biashara ya Youtube Account.
Kumiliki account ya youtube au Channel ya Youtube ni jambo moja na kufanya account yako ya youtube kuanza kuingiza pesa (kulipwa) ni jambo jingine sasa leo kwenye hii article tunaenda kuelezea mchakato mzima hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza youtube channel na utaratibu mzima wa kujiunga na youtube monetisation na hatimaye kuanza kulipwa pesa, hapahapa bongo wapo watu wanalipwa na youtube hadi milioni 10 na zaidi kwahiyo this is real business.
Kwanini ni muhimu kila mtu kuwa na youtube account
Kama nilivyosema youtube ni biashara ambayo unaanzisha bure kabisa kinachotakiwa ni bundle, sasa youtube unaruhusiwa kuweka maudhui (videos) yua aina yeyote ile ilimradi yasipingane na sheria za kupost videos youtube, Youtube hawaruhusu maudhui ya ngono, mauaji, na mambo ya hatari ambayo youtube wameainisha hapa
Kila mtu ana uwezo ktk jambo fulani ambalo anaweza kulizungumzia au kulifanya akiwa LIVE au Akijirekodi iwe ni kutoa ELIMU fulani, Maelekezo fulani, Utaratibu fulani, Historia fulani, au Jambo lolote lile liwe la Kuelimisha au Kufurahisha/Kuchekesha haijalishi ilimradi usivunje zile sheria za youtube na za nchi pia.
Soma Hii: Jinsi ya kufungua facebook page na utaratibu wa kulipwa.
Kila mtu anaweza kufanya hii kitu kwa sababu kila mwanadamu kuna sekta anaifahamu na anaweza kumuelewesha mwingine aelewe pia, kama wewe ni msusi wa nywele, mfugaji wa kuku, mkulima, mpishi, muuza duka, fundi nyumba au nyingine yeyote ile fahamu kwamba hakuna kinachokuzuia kumiliki biashara ya Youtube channel kwa bure kabisa na kupost contents.
Jinsi ya kufungua Youtube Channel
Jinsi ya kufungua Youtube Channel kigezo cha kwanza lazima uwe na Google Account au Gmail Acount hii ni email yako ambayo unaifungua hapa kumbuka Youtube inamilikiwa na Google LLC. Kufungua Google account ni bure kabisa, sasa ukiwa tayari unayo Google Account hatua inayofuata ni kwenda kufungua youtube channel (inakuwa inashikiliwa na hii google account uliyotengeneza).
Kufungua Youtube Channel Nenda kwenye App ya Youtube direct au unaweza kwenda Google kisha ukasearch Youtube itakuja link ya kwanza itakua youtube utabonyeza na itakupeleka Youtube Homepage utaona videos za watu wengine zimetawala kwenye homepage ya youtube Hapo utaangalia upande wa kuli juu kabisa kuna TAB (kwenye picha yako ndogo) chini yake pameandikwa CREATE CHANNEL Utabonyeza hapo na utatokea ukurasa unajaza majina ya channel yako pamoja na picha (Profile picture, Cover photo).

Nini Cha Kupandisha kwenye Channel yako mpya
Baada ya kutengeneza channel yako mpya kitu kikubwa kinachokuja sasa ni swala la NICHE, Ni video za aina gani utakuwa uapandisha kwenye channel yako, kama nilivyosema kila mtu anastahili kumiliki youtube channel, kwa sababu kila mtu kuna sehemu anayoifahamu, kuna jambo lolote mtu atakuwa analifahamu na ana uwezo wa kulielezea kwa wengine,
Angalia unapenda nini inaweza kuwa chchote kile magari, uvuvi, uwindaji, kuchoma nyama, kuogelea, kufanya mazoezi mamabo ya kufanya ni mengi sana in short kila kitu unachofanya kwenye maisha yako ya kawaida unaweza kukifanya pia kwenye channel yako ilimradi usivunje sheria za nchi, pamoja na sheria za Youtube
Hapa unatakiwa kuwa MBUNIFU kwa sababu kila kitu tayari kuna watu wanafanya walishaanza muda mrefu kabla yako lkn uzuri wa youtube hata ukiwa creator mdogo bado una nafasi ya kuwafikia watu (viewers) wengi zaidi kutokana na jinsi Youtube Algarithm zinavyofanya kazi ndio maana nasema hapa unatakiwa kuwa mbunifu kama ambavyo ukifungua duka la nguo au mama ntilie lazima utajaribu kuwa na ubunifu fulani ili uweze kuwin wateja wengi,
Vivyo hivyo ukifungua Youtube channel mpya unatakiwa kuwa na ubunifu kweli means unatakiwa kutengeneza videos (contents) kwa ubora na ubunifu na upekee ili upate views nyingi kumbuka video ikipata views na engegement nzuri youtube watasuggest kwa watu wengi zaidi hiyo video huku hakuna uchawi ni facts, watu wa mwanzo waki view video yako dakika kadhaa youtube inaamini hiyo video ni nzuri na inafaa kwa watu wengi hivyo wanaipeleka kwa watu wengi zaidi na kama ikiwa kweli nzuri unatoboa inshu kubwa hapa ni kujiongeza UBUNIFU KWENYE KAZI ZAKO.
YouTube Monetization (YouTube Partner Program -YPP)
Ili uanze kulipwa na Youtube unahitaji kujiunga kwenye mfumo wa malipo wa youtube (YouTube Partner Program -YPP) sasa ili ukubaliwe kwenye huu mfumo wa Youtube monetization unatakiwa uwe na SUBSCRIBERS 1000 na MASAA (WATCH HOURS) 4000 Ndani ya siku 365. Vigezo vyote hivi vitoke kwenye contents (videos) unazopandisha kila siku na hata ukitimiza hivi vigezo ndani ya mwezi mmoja youtube hawana shida wanakupa matangazo (monetization).

Baada ya kutimiza hivi vigezo hatua inayofuata ni kutuma maombi ya kuwashiwa matangazo kwenye channel yako (YouTube Partner Program -YPP) maombi huwa yanachukua siku 7 na zaidi, Utatakiwa kufungua account ya Google Adsense (matangazo ya google)na utatakiwa kuverify hii account ya ADSENSE Kupitia CODE maalum (Utatumiwa na google kwenye sanduku la posta) hii huchukua hadi wiki 2 au 3 kwa sababu ni Barua yenye hiyo CODE na inatumwa moja kwa moja kutoka makao makuu ya Google LLC.
Baada ya kuipata hiyo code na kuverify utajaza fomu za TAX hivi vyote utavipata kupitia YOUTUBE STUDIO – Hii ni website maalumu kwa Youtube creators kama wewe kwenye hiyo website/App ndio utaweza kuona analytics namna jinsi video mbalimbali zinavyoperform ktk channel yako, kupandisha videos na kuedit, kwa ufupi kwenye STUDIO ndio sehemu maalum ya kufanya management ya videos na channel yako kwa ujumla.

Malipo yanatokana na views zako
Ukiwa umetimiza vigezo na upo tayari kulipwa sasa hapa mahesabu mengine yanakuja kwamba unalipwa vipi? Well, Unalipwa kutokana na VIEWS amabazo videos zako zinapata huko online more views more money, Kwahiyo kitu kikubwa ni kuhakikisha unapata views nyingi kwa sabbu ndio pesa yenyewe – maana ukishaunganishwa kwenye mfumo wa monetization kila video yako inawekewa matangazo kadri watu wanavyoangalia video zako watapata kuona matangazo ambayo Aliyetangaza (Advertiser) ameyalipia kwa YouTube na hivyo Youtube wanagawana hiyo pesa na wewe (Content Creator).
Kiasi cha kulipwa kinategemea vitu vingi kama nchi wanapotoka viewers wako, umri wa viewers wako, na jinsi nwalivyo Engage na matangazo yaliyopo kwenye videos zako. Lakini pesa hadi ifike dola $100 ndio utaweza kuitoa (kutumwa kwenda bank)