Jinsi ya Kuhuisha Taarifa na Kuangalia Status ya Maombi ya Kazi Kupitia Ajira Portal Tanzania
Waombaji wa ajira serikalini kupitia Ajira Portal wanakumbushwa kuhakikisha taarifa zao zimehuishwa (updated) ili kuendana na mahitaji mapya ya mfumo. Kwa mwaka 2025, mfumo wa Ajira Portal umeongeza mahitaji ya taarifa mahsusi zinazotakiwa kuwepo kabla ya kuendelea na kutuma maombi ya kazi.
Kuhuisha Taarifa za Mtumiaji (User Profile Update)
Kabla ya kutuma maombi yoyote ya kazi mpya, unatakiwa kuhuisha taarifa zako katika sehemu zifuatazo:
1. Personal Details
Katika sehemu hii, unatakiwa kuthibitisha au kuongeza Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN). Hili ni sharti la lazima kwa waombaji wote wa kazi serikalini. Bila kuweka NIN, mfumo hautaruhusu kutuma maombi.
👉 Hatua:
- Ingia kwenye akaunti yako ya Ajira Portal kupitia: https://portal.ajira.go.tz
- Bonyeza “Profile” > “Personal Details”
- Jaza au thibitisha NIN yako
- Hakikisha taarifa nyingine kama jina, jinsia, tarehe ya kuzaliwa n.k. ziko sahihi
2. Academic Qualifications
Eneo hili linahusu taarifa zako za elimu. Unatakiwa kuweka kila kozi (program) kwenye ‘Category’ sahihi ili mfumo uweze kutambua sifa zako ipasavyo.
Mifano ya Category:
- Kozi ya “Law” iwe kwenye category ya Legal
- Kozi ya “Nursing” iwe kwenye category ya Health
- Kozi ya “ICT” iwe kwenye category ya Information Technology
Kumbuka: Maombi mengi hukataliwa au kupuuzwa kutokana na kozi kutowekwa kwenye category sahihi.
Jinsi ya Kuangalia ‘STATUS’ ya Maombi Yako ya Kazi
Ajira Portal inakuwezesha kuona hali ya kila ombi ulilowahi kutuma. Hili linakusaidia kujua kama:
- Umepangiwa usaili
- Hukuitwa, na sababu yake
- Ombi lako liko kwenye hatua gani
Hatua:
- Ingia kwenye akaunti yako: portal.ajira.go.tz
- Nenda kwenye menyu upande wa kushoto na bonyeza “My Application”
- Katika ukurasa huu utaona:
- Jina la kazi uliyotuma
- Tarehe ya kutuma maombi
- Status ya ombi hilo (Mfano: “Called for Interview” au “Not Selected”)
- Sababu ya kukataliwa kama hukuchaguliwa
Sababu Zinazoweza Kusababisha Kukosa Usaili
Baadhi ya sababu zinazojitokeza mara kwa mara kwa waombaji ambao hawachaguliwi ni:
- Kozi haikuwekwa kwenye category sahihi
- Taarifa za elimu hazikuwekwa kikamilifu
- Kukosekana kwa NIN kwenye profile
- Taarifa za mawasiliano si sahihi
- Kutokuwepo kwa vyeti vilivyowekwa kwenye mfumo (PDF)
Hitimisho
Kwa mafanikio kwenye maombi ya kazi serikalini, ni lazima uhakikishe:
- Taarifa zako kwenye Ajira Portal zimekamilika
- Umepitia My Application kila baada ya kutuma maombi
- Unajua sababu zinazoweza kukunyima nafasi ili uzirekebishe mapema
👉 Usisubiri siku ya mwisho! Huhisha taarifa zako mapema ili kuwa tayari kwa fursa yoyote mpya ya ajira serikalini.