Jinsi ya Kuomba Kujiunga na Chuo cha Ardhi (ARU)
Jinsi ya Kuomba Kujiunga na Chuo cha Ardhi Dar es Salaam (ARU)
Mwongozo wa kina kwa waombaji wa Degree, Diploma na Postgraduate Programmes
Sifa za Kujiunga na Chuo cha Ardhi
Kabla ya kuanza mchakato wa maombi, ni muhimu kuhakikisha unakidhi sifa zinazohitajika kwa kozi unayotaka:
- Shahada ya Kwanza: Principal Pass mbili ACSEE au Diploma husika.
- Stashahada: D tatu (3) katika CSEE au sifa mbadala zinazokubalika na NACTVET.
- Postgraduate: Shahada ya kwanza yenye GPA ya angalau 2.7 au zaidi.
Tembelea Tovuti Rasmi ya ARU
Fungua tovuti ya www.aru.ac.tz kupata taarifa rasmi kuhusu udahili na kozi zinazotolewa.
Fungua Akaunti ya Maombi Mtandaoni
Tembelea admission.aru.ac.tz ili kuanzisha akaunti yako:
- Bofya “Apply Now” kwenye ukurasa wa mwanzo.
- Jaza taarifa binafsi na ujisajili.
- Ingia kwenye akaunti na uanze kujaza fomu ya maombi.
Chagua Kozi Unayotaka
Chagua programu unayotaka kujiunga nayo kulingana na kiwango chako cha elimu na sifa zako. Soma vizuri mahitaji ya kila kozi kabla ya kuchagua.
Upload Nyaraka Muhimu
Andaa na upload nyaraka zifuatazo:
- Cheti cha CSEE na/au ACSEE
- Transcript ya Diploma/Shahada
- Picha ya pasipoti
- Namba ya NIDA au kitambulisho
Lipia Ada ya Maombi
Ada ya maombi ni kati ya TSh 10,000 – 30,000. Lipa kupitia control number utakayopewa na hakikisha unathibitisha ndani ya mfumo.
Subiri Majibu ya Udahili
Baada ya kukamilisha maombi, angalia status yako kupitia akaunti ya admission au kupitia orodha za waliochaguliwa kwenye tovuti ya ARU na TCU.
Thibitisha Udahili
Ukichaguliwa, fuata taratibu za kuthibitisha udahili kupitia TCU (kwa waombaji wa shahada) au kwa moja kwa moja ARU (kwa diploma/postgraduate).
Jiandae kwa Usajili Chuoni
Andaa vitu muhimu kama:
- Fomu za usajili zilizojazwa
- Malipo ya ada
- Hati halisi za masomo
- Maelekezo ya makazi (hosteli)
Makala Zinazohusiana na Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU)
- Sifa za Kujiunga na Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU)
- Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu cha Ardhi 2025/2026
- Jinsi ya Kuthibitisha Usahili Chuo Kikuu cha Ardhi
- Jinsi ya Kutumia E-Learning Portal ya Chuo cha Ardhi
- Ada na Gharama za Masomo Chuo Kikuu cha Ardhi
- Jinsi ya Kuomba Kujiunga na Chuo Kikuu cha Ardhi
Hitimisho
Kujiunga na Chuo cha Ardhi ni fursa ya kipekee ya kujifunza kwa vitendo katika sekta zinazohusiana na ardhi na maendeleo ya miji. Fuata hatua zote zilizoelezwa kwa umakini ili kuongeza nafasi ya kupokelewa chuoni.