Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima
Cheti cha kuzaliwa ni hati maalum na ni haki ya kila raia wa nchi ya tanzania kuwa nacho. Cheti cha kuzaliwa ndio ushahidi wa kwamba wewe ni mtanzania halisi, kikionyesha taariza zote za mtu husika kuanzaia tarehe, mahali, na wazazi wake. Hati hii hutumika katika nyanja mbalimbali za maisha, kuanzia kutambulisha mtu, kusafiri, kupata ajira, mashuleni hadi kufungua akaunti za benki.
Cheti cha kuzaliwa kwa mtoto ni rahisi sana kukipata kwa sababu huwa kinatolwa mara baada tu ya mtoto kuzaliwa, lakini kwa bahati mbaya kuna baadhi ya situation kwenye maisha zinatokea na unakuta mzazi anakosa cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake.
Hali hii inasbabishwa na mambo mengi kama vile uzembe, ugonjwa, mzazi kutoona umuhimu wa cheti hii imetokea sana miaka ya nyuma,
Sasa kama ambavyo tumeona umuhimu wa cheti ni hasara sana kwa kijana au mtu mzima sasa kutokuwa na cheti au kukosa cheti, kwa sabbu itakuweka mbali na fursa nyingi zikiwemo fursa za ajira za serikali pia binafsi maana cheti ndio hati maalum ya uraia wako (Tanzania)
Kwenye hii article tunaenda kuangalia utaratibu maalum wa kiserikalin wa kpata cheti cha kuzaliwa kwa kijana au mtu mzima,
Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Tanzania
Kama tulivyosema mtu anaweza kukosa cheti cha kuzaliwa kutokana na sababu mbalimbali sasa ufuatao ndio utaratibu rasmi wa kiserikali wa namna jinsi ya kuomba cheti cha kuzaliwa,
Haya ndio matumizi mbalimbali ya cheti cha kuzaliwa
- Kupata hati ya kusafiria (pasipoti)
- Kuandikishwa kupiga kura
- Kuomba ajira
- Kuomba mikopo
- Kufungua akaunti ya benki
Utaratibu wa Kupata Cheti cha Kuzaliwa Tanzania
- Jaza Fomu ya Usajili wa Kizazi, B3 (ipatikane kwenye ofisi za RITA au mtandaoni).
- Ambatanisha picha ya mtoto (passport size) na nyaraka zinazohitajika (kadi ya kliniki, cheti cha ubatizo, barua kutoka serikali za mitaa, vyeti vya shule, n.k.).
- Kwa wale waliozaliwa zamani sana, utahitaji pia kadi ya taifa, kadi ya kupigia kura, au bima ya afya.
- Lipa ada ya shilingi 20,000.
Nyaraka za Ushahidi: Mzazi au mlezi anatakiwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali kama vile:
- Kadi ya kliniki ya mtoto
- Cheti cha ubatizo (ikiwa kipo)
- Barua kutoka mamlaka za serikali (mfano, ofisi ya mtendaji wa kata/kijiji)
- Cheti cha kumaliza elimu ya msingi au sekondari
Nyaraka za Utambulisho (kwa waliozaliwa zamani): Kwa wale waliozaliwa miaka mingi iliyopita, wanatakiwa kuambatanisha nyaraka za ziada kama vile:
- Kadi ya Utaifa pamoja na Kadi ya Kura au Bima ya Afya.
- Leseni ya Gari (lazima iambatane na Kadi ya Utaifa au Kadi ya Kura).