Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA | Njia rahisi ya Kuangalia Namba ya NIDA kwenye Simu.
Namba ya NIDA (National Identification Number). Ni namba muhimu sana inayokutambulisha wewe kama mtanzania halisi(wa kuzaliwa) kitambulisho hichi hutumika sehemu mbalimbali kuverify uraia wako mfano kupata verifications kwenye platforms mbalimbali au mitandaoni, Usajili mashuleni, Kujaza fomu za mikopo na hata kuomba ajira baadhi ya sehemu, n.k.
Kupata namba ya NIDA moja kwa moja kwenye simu yako kuhakikisha huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinapatikana kwa urahisi. Ni njia rahisi na ya haraka ambayo inawawezesha watu wengi zaidi kupata huduma muhimu bila kulazimika kusafiri umbali mrefu au kusubiri kwa muda mrefu kwenye foleni katika ofisi ya NIDA.
Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2025
Kupata namba ya NIDA kumekuwa rahisi zaidi kuliko hapo awali. Sasa mtu yeyote anaweza kupata namba ya NIDA kwa urahisi na haraka kupitia simu ya mkononi, bila kujali mahali alipo au aina ya simu anayotumia. Hadi hivi sasa kuna njia kuu mbili za kupata namba ya NIDA kwa kutumia simu ya mkononi. Njia hizi ni kama zifuatazo;
- Kupitia USSD: Huu ni mfumo unaokuwezesha kuingiliana na kompyuta ya NIDA kwa kutumia misimbo maalumu. Ni njia rahisi na ya haraka ambayo haihitaji muunganisho wa intaneti.
- Kupitia SMS: Njia hii inahusisha kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba maalum ya NIDA. Kama ilivyo kwa USSD, njia hii pia haihitaji muunganisho wa intaneti.
Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia USSSD
USSD (Unstructured Supplementary Service Data) ni njia rahisi na ya haraka ya kupata namba ya NIDA bila kuhitaji muunganisho wa intaneti. Fuata hatua hizi rahisi:

- Piga *152*00# kwenye simu yako ya mkononi.
- Chagua namba 3 (Ajira na Utambuzi).
- Chagua namba 2 (NIDA).
- Ingiza majina yako matatu (3) uliyojisajili (Mfano: Dan John Sele).
- Ingiza namba ya simu uliyojaza kwenye fomu ya maombi (Mfano: 0XXXXXXX).
- Kubali ombi lako.
- Utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye namba yako ya NIDA.
Huduma hii kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa Airtel na Vodacom.
Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia SMS
Njia nyingine rahisi ya kupata namba yako ya NIDA ni kupitia SMS. Fuata hatua hizi:
- Andika ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye majina yako matatu (3) uliyojisajili (Mfano: Dan John Sele).
- Tuma SMS hiyo kwenda namba 15096.
- Utapokea ujumbe wa kujibu wenye namba yako ya NIDA. Huduma hii ni bure na inapatikana kwa mitandao yoteya simu nchini Tanzania.