Sasa ni rahisi sana kuangalia namba yako ya NIDA online wakati wowote kwenye smartphone yako, kwenye hii article tunaenda kuangalia utaratibu mzima wa namna ambavyo unaweza kuangalia namba yako ya NIDA mtandaoni.
Umuhimu wa NIDA kwako
Kitambulisho cha NIDA (National Identification Authority) ni hati halali inayomilikiwa na mzaliwa wa Tanzania. Kitambulisho hichi ndicho kinatumika kama uthibitisho wa uraia na utambulisho wa mtu. Kitambulisho cha NIDA Kinahitajikaga maeneo mengi sana kwa mfano:
- Huduma za Kibenki: Ili kufungua akaunti au kupata mikopo.
- Ushiriki Katika Uchaguzi: Ili kutekeleza haki ya msingi ya kupiga kura.
- Huduma za Serikali: Ili kupata huduma mbalimbali za serikali.
- Miamala Mingine Muhimu: Kama vile kununua ardhi, kusajili ndoa, na kupata leseni.
- Kusajili Laini za Simu: Namba ya kitambulisho cha NIDA ni lazima wakati wa kusajili laini ya mtandano wa simu yeyote
Kuangalia Namba ya NIDA Online
Fuatana na mwandishi wa makala hii kuangalia njia rahisi ndani ya muda mfupi tu utakua tayari umefahamu namna jinsi ya kuangalia Namba yako ya NIDA online.
Utaratibu Kuangalia Namba ya NIDA Online
1. Tembelea Tovuti Rasmi: Fungua kivinjari chako cha wavuti na uende kwenye tovuti rasmi ya NIDA: https://services.nida.go.tz/nidportal/get_nin
2. Toa Taarifa Zinazohitajika: Jaza kwa usahihi taarifa zifuatazo:
- Jina la kwanza
- Jina la mwisho
- Tarehe ya kuzaliwa
- Jina la kwanza la mama
- Jina la mwisho la mama
3. Thibitisha Wewe Sio Roboti: Andika neno linaloonyeshwa kwenye picha ili kuthibitisha kuwa wewe si roboti.
4. Pata Namba ya NIDA: Bofya kitufe cha “Angalia” ili kupata namba ya NIDA.
