Matokeo ya Darasa la Saba na Shule walizopangiwa 2025
Baraza la Usimamizi wa Mitihani ya Taifa (NECTA) limezitangaza rasmi matokeo ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi kwa mwaka 2025. Matokeo haya ni ya darasa la saba na yameorodhesha shule walizopangiwa vijana waliofaulu kuendelea na elimu ya sekondari. Hii ni hatua muhimu kwa wanafunzi, wazazi, na walezi ili kupanga mipango ya elimu ya sekondari kwa mwaka ujao.
NECTA inasisitiza umuhimu wa kufatilia matokeo haraka iwezekanavyo. Wazazi na walezi wanashauriwa kuhakikisha wanafuatilia matokeo ya watoto wao mara moja ili kujua ni shule gani zimepangiwa. Hii itasaidia kuandaa masuala ya uhamisho wa wanafunzi, uandikishaji, na maandalizi ya kuanza mwaka wa masomo wa sekondari bila kuchelewa.
Kutazama matokeo ya darasa la saba 2025 ni rahisi. Tembelea tovuti rasmi ya NECTA kisha bofya kiunganishi cha Matokeo. Chagua aina ya elimu “PSLE”, kisha chagua Mkoa na Wilaya uliyosoma. Mwisho, chagua shule ya msingi uliyohitimu ili kupata orodha kamili ya matokeo kutoka shule yako.
Matokeo haya ni nyenzo muhimu kwa kupanga maisha ya shule ya sekondari ya mwanafunzi. Hakikisha unafuatilia matokeo kwa wakati ili kuweza kuandaa masuala ya uhamisho, usajili, na maandalizi mengine muhimu.


AJIRA UPDATES > WHATSAPP