Nafasi ya Kazi: Mtaalamu wa Sosholojia (Sociologist) – TANROADS Septemba 2025
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) unahusika na kusimamia mtandao wa barabara kuu za taifa pamoja na maendeleo ya viwanja vya ndege katika Tanzania Bara. Majukumu yake ni pamoja na kupanga, kubuni, kujenga na kutunza barabara ili kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kutumia wataalamu wenye weledi. Aidha, TANROADS husimamia shughuli za udhibiti wa mizigo kupitia mizani za barabarani.
Meneja wa Kanda wa TANROADS Shinyanga, kwa niaba ya Mtendaji Mkuu, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na ujuzi wa kutosha kujaza nafasi kwa ajili ya mradi wa “Kuboresha Barabara ya Kahama – Bulyanhulu – Kakola (73KM) kuwa kiwango cha lami” chini ya Mkataba Na. TRD/HQ/1057/2023/24.
Nafasi Inayotangazwa
Sociologist (Mtaalamu wa Sosholojia) – Nafasi 1
Sifa za Muombaji
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na Shahada ya Kwanza katika moja ya fani hizi: Social Work, Social Welfare, Sociology, Guidance and Counseling au taaluma inayofanana kutoka chuo kinachotambulika.
- Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili (2) katika kazi zinazohusiana.
Majukumu ya Msingi
- Kupitia na kuhakikisha utekelezaji wa Construction Environmental and Social Management Plan (C-ESMP) unazingatia Social Management Plan (EMP) ya mradi.
- Kusimamia utekelezaji wa Resettlement Action Plan (RAP) na mipango mingine ya kijamii.
- Kuanzisha na kuendesha mfumo wa kushughulikia malalamiko (Grievance Redress Mechanism – GRM) na kuhakikisha unafanya kazi ipasavyo.
- Kuratibu ushiriki wa jamii za wenyeji katika masuala yanayohusiana na mradi.
- Kufuatilia na kutathmini Social Impact Assessment (SIA) ili kubaini na kupunguza athari za kijamii zinazoweza kujitokeza.
- Kushirikiana na taasisi na wadau husika kuhusu masuala ya kijamii.
- Kufanya majukumu mengine yoyote yatakayoelekezwa na Meneja wa Mradi.
Masharti ya Ajira
- Mkataba wa ajira ni wa mwaka mmoja wenye uwezekano wa kuongezwa kulingana na maendeleo ya mradi.
- Mshahara utalipwa kwa kuzingatia ngazi za mishahara za TANROADS, pamoja na posho za eneo la kazi kulingana na sera ya motisha ya TANROADS.
- Waombaji waliopata nafasi lazima wawe tayari kufanya kazi muda mrefu katika Wilaya ya Kahama, ambako mradi unatekelezwa.
Jinsi ya Kuomba
Waombaji wote waliokidhi vigezo wanapaswa kuwasilisha:
- CV (Curriculum Vitae) yenye maelezo ya kina na iliyosainiwa
- Nakili zilizothibitishwa za vyeti vya elimu
- Majina ya wadhamini (referees) wawili wanaoaminika pamoja na anuani zao, namba za simu na barua pepe
⏰ Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 6 Oktoba 2025 saa 10:30 jioni.
📮 Tuma maombi kwa anuani hii:
The Regional Manager
TANROADS
P.O. Box 62
Shinyanga
Angalizo
- Maombi yatakayowasilishwa baada ya muda uliopangwa hayatazingatiwa.
- Ni waombaji walioteuliwa pekee watakaopigiwa simu kwa usaili.
- Wale wasioitwa kwenye mahojiano watambue kuwa hawakufanikiwa.