Nafasi za Kazi: Dereva Daraja la II – Nafasi 8
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga – Septemba 2025
Muda wa Maombi: Kuanzia 18/09/2025 hadi 01/10/2025
Majukumu ya Kazi
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha usalama wake.
- Kuwasafirisha watumishi kwenda maeneo mbalimbali kwa shughuli za kikazi.
- Kufanya marekebisho madogo ya gari yanayohitajika.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kurekodi na kuhifadhi taarifa za safari zote kwenye logbook.
- Kuhakikisha gari lipo safi wakati wote.
- Kufanya majukumu mengine atakayopangiwa na msimamizi wake.
Sifa za Mwombaji
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
- Awe na leseni halali ya daraja la E au C.
- Awe na uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika kazi ya udereva bila kusababisha ajali.
- Awe amehitimu mafunzo ya msingi ya ufundi stadi (mfano VETA) au taasisi nyingine inayotambulika na Serikali.
Maslahi
Kiwango cha mshahara: TGS B kwa mujibu wa ngazi za mishahara za Serikali.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Hii ni ajira ya muda wote (Full-time).
Kwa maombi tafadhali tembelea kiunganishi kilicho rasmi cha Ajira Portal kupitia link hapa chini: