Nafasi za Kazi: Madereva (Nafasi 22) – Mtibwa Sugar Estates Ltd | Julai 2025
Taarifa ya Kampuni
Mtibwa Sugar Estates Limited ni kampuni inayojihusisha na kilimo na usindikaji wa miwa, iliyopo katika eneo la Mtibwa–Turiani, Wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro. Kampuni hii inajivunia utamaduni wa mshikamano kazini, kusaidiana, na kukuza vipaji vya wafanyakazi wake. Mfanyakazi yeyote anayekaribishwa Mtibwa Sugar huwa sehemu ya familia inayojali ustawi wa kila mmoja.
Nafasi za Kazi: Madereva – Nafasi 22
Kampuni inatangaza nafasi 22 za ajira kwa madereva wa magari ya kusafirisha wafanyakazi (labour trucks) na magari ya mizigo mizito (dumper trucks) kwa ajili ya shughuli zake ndani ya eneo la Mtibwa Sugar.
Sifa za Waombaji
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na umri wa chini ya miaka 40.
- Awe na leseni halali ya kuendesha magari makubwa au ya abiria.
- Awe tayari kuishi eneo la Mtibwa.
- Awe tayari kuanza kazi kati ya Agosti hadi Septemba 2025.
- Awe na uzoefu wa angalau miaka 5 ya udereva.
- Asiwe na rekodi ya makosa ya jinai au ya usalama barabarani.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia mojawapo ya njia zifuatazo:
- Barua pepe: Hr@mtibwa-sugar.co.tz
- Kwa mkono: Wasilisha maombi katika ofisi za HR – MTIBWA
- Kwa barua: Tuma kupitia posta kwa anwani iliyo hapa chini
Maombi yaambatane na:
- Curriculum Vitae (CV)
- Picha ndogo (passport size)
- Nakala ya leseni ya udereva
- Cheti cha mafunzo ya udereva
- TIN (Namba ya mlipakodi)
- Kitambulisho cha NIDA au kadi ya mpiga kura
- Cheti cha kuzaliwa
Anwani ya Kutuma Maombi
Human Resources and Administration Manager
Mtibwa Sugar Estates Limited
P.O. Box 42,
Mtibwa – Morogoro
Mwisho wa Kutuma Maombi:
25 Julai 2025
Kumbuka: Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe hiyo hayatazingatiwa. Hakikisha umeambatanisha nyaraka zote muhimu.