Nafasi za kazi Zilizotangazwa Leo Ajira Portal 2025
Ajira Portal ni mfumo rasmi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaosimamiwa na Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Mfumo huu hutumika kutangaza nafasi za ajira na kurahisisha mchakato wa kutuma maombi ya kazi katika taasisi mbalimbali za umma. Kwa mwaka 2025, Ajira Portal imeendelea kuwa njia ya msingi kwa Watanzania wanaotafuta ajira serikalini.
Kupitia makala hii, utapata taarifa muhimu kuhusu nafasi mpya za kazi zilizotangazwa, jinsi ya kujisajili na kutuma maombi kupitia Ajira Portal, pamoja na vidokezo muhimu vya kuhakikisha maombi yako yanakubalika kwa mafanikio.
Nafasi Mpya za Kazi Kupitia Ajira Portal – 2025
Kila siku, Ajira Portal hupokea matangazo ya ajira kutoka:
- Wizara mbalimbali (Afya, Elimu, Kilimo, Uchukuzi n.k.)
- Halmashauri na Manispaa
- Vyuo vya Serikali
- Hospitali za Umma
- Mashirika ya Umma
Zifuatazo ni nafasi mpya za kazi zilizotangazwa wiki hii :
Kwa orodha kamili ya nafasi zote, tembelea tovuti ya Ajira Portal: https://portal.ajira.go.tz
Jinsi ya Kujiunga na Ajira Portal (Kujisajili)
- Tembelea tovuti rasmi: https://portal.ajira.go.tz
- Bonyeza “Register” au “Jisajili”
- Jaza taarifa binafsi: Jina, Namba ya NIDA, barua pepe, namba ya simu
- Chagua username na password
- Thibitisha kupitia email utakayotumiwa
- Login kutumia email/username na password
Jinsi ya Kutuma Maombi ya Kazi Kupitia Ajira Portal
- Ingia kwenye akaunti yako
- Jaza profile kikamilifu: Elimu, uzoefu, vyeti, lugha n.k.
- Nenda sehemu ya “Vacancies”
- Tafuta kazi unayotaka, soma tangazo lake
- Hakikisha sifa zako zinakidhi
- Bonyeza “Apply” na thibitisha maombi
Vidokezo Muhimu
- Hakikisha profile imekamilika kabla ya kutuma maombi
- Tumia kompyuta badala ya simu ili kuepuka makosa
- Vyeti viwe kwenye mfumo wa PDF
- Tuma mapema – usisubiri siku ya mwisho
Umesahau Password ya Ajira Portal?
- Nenda kwenye https://portal.ajira.go.tz
- Bonyeza “Forgot Password?”
- Weka email uliyosajili nayo
- Fungua email na fuata link ya kuweka password mpya
Kwa taarifa zaidi kuhusu nafasi mpya na walioitwa kazini: