Nauli ya Treni ya Umeme ya SGR Dar -Dodoma
Watanzania tumeendelea kufaidi matumizi ya treni za kisasa kusafiri safari za ndani treni hizi ambazo ni “express train,” zinatoa huduma za kisasa na za haraka, Zimesaidia sana kuendesha uchumi wa nchi na kuharakisha maendeleo kwa kiasi kikubwa. Hadi sasa ni treni za abiria pekee ndio zimeshafika na zinafanya kazi kwa safari mbalimbali ndani ya nchi.
Ratiba ya Safari na Vituo Treni ya Umeme ya SGR Dar to Dodoma
Treni za Umeme za SGR zimeanza safari zake za Dar kwenda Dodoma rasmi Julai 25, Mwaka jana. Treni hizi zinaanza safari Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na kufika Dodoma saa 3:25 usiku, ikimaanisha safari nzima itachukua saa tatu na dakika 25 pekee.
Treni hii itasimama Morogoro pekee kabla ya kuendelea na safari hadi Dodoma. Kwa abiria wanaosafiri na treni ya kawaida , safari zitaanza saa 3:30 asubuhi kutoka Dar es Salaam na kufika Dodoma zitasimama katika kituo cha Pugu.
Nauli ya Treni ya Umeme ya SGR Dar – Dodoma
Nauli za treni ya SGR zinatofautiana kuna madaraja tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya abiria husika kuna economy class, business class
Treni ya Kawaida
SAFARI | DARAJA | GHARAMA |
---|---|---|
DAR – DODOMA | KAWAIDA | Tsh 37,000 |
Treni ya Haraka (Express Train)
SAFARI | DARAJA | GHARAMA |
---|---|---|
DAR – DODOMA | Daraja la Biashara (Business Class) | Tsh 70,000 |
DAR – DODOMA | Daraja la Juu (Royal Class) | Tsh 120,000 |
Upatikanaji wa Tiketi za Treni ya Umeme ya SGR Dar – Dodoma
Tiketi za treni zote zinapatikana kwa njia ya mtandao (online) kupitia tovuti rasmi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na pia katika stesheni za SGR.
Soma Hii: Nauli mpya za Treni ya Umeme SGR Tanzania 2025
