Tangazo la Nafasi 137 za Kazi Serikalini Kupitia UTUMISHI – July 2025
Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetoa tangazo jipya la ajira zenye jumla ya nafasi 137, zilizotolewa kwa taasisi mbalimbali za serikali. Tangazo hili limetolewa rasmi tarehe 12 Juni 2025, likihusisha taasisi sita ikiwemo TEMESA, TANROADS, TPSC, LGTI, TICD na TAA.
Kama wewe ni Mtanzania mwenye sifa stahiki na ndoto ya kuhudumu serikalini, huu ni wakati wako wa kuchukua hatua. Hapa chini tumekuletea muhtasari wa nafasi zilizo wazi pamoja na sifa kuu zinazohitajika.
1. Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA)
Jumla ya nafasi: 32
Engineer II (Marine) – Nafasi 2
Ferry Captain II – Nafasi 15
Technician II (Mechanical) – Nafasi 15
Sifa:
Waombaji wanapaswa kuwa na Shahada au Stashahada (Diploma) katika fani za Uhandisi wa Mitambo au Uhandisi wa Majini, pamoja na usajili wa kitaaluma kwa wahandisi.
2. Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)
Jumla ya nafasi: 81
Land Surveyor II – Nafasi 2
Valuer II – Nafasi 2
Weighbridge Officer II – Nafasi 50
Assistant Laboratory Technician II – Nafasi 10
Dereva Daraja la II – Nafasi 15
Receptionist II – Nafasi 2
Secretary II (OM) – Nafasi 2
Sifa:
Kiwango cha elimu kinatofautiana kati ya Shahada, Diploma na Cheti kutegemea nafasi. Kwa madereva, uzoefu unaongezea nafasi ya kuchaguliwa.
3. Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)
Jumla ya nafasi: 10 (Wakufunzi Wasaidizi – Assistant Lecturers)
Hisabati / Takwimu – Nafasi 4
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) – Nafasi 2
Sheria – Nafasi 2
Ununuzi na Usimamizi wa Ugavi – Nafasi 4
Ujuzi wa Mawasiliano – Nafasi 2
Sifa:
Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Uzamili (GPA ≥ 3.8) na Shahada ya Kwanza (GPA ≥ 3.5) katika maeneo husika.
4. Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa (LGTI)
Jumla ya nafasi: 3
Assistant Lecturer – Public Administration – Nafasi 1
ICT Officer II (Programming) – Nafasi 2
Sifa:
Kwa nafasi ya mhadhiri, Shahada ya Uzamili inahitajika; kwa ICT Officer, Shahada ya kwanza katika Tehama/Programming inatosha.
5. Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD)
Jumla ya nafasi: 5 (Wakufunzi Wasaidizi – Tangazo la Marudio)
Sociology – Nafasi 1
Community Development – Nafasi 3
Social Work – Nafasi 1
Sifa:
Shahada ya Uzamili (GPA ≥ 3.8) na Shahada ya kwanza (GPA ≥ 3.5) kwenye taaluma husika zinahitajika.
6. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
Jumla ya nafasi: 2
Assistant Aircraft Marshaler – Nafasi 2
Sifa:
Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Rasilimali Watu, Takwimu, Biashara au fani inayofanana.
Fungua Fursa Yako Leo!
Ikiwa unaamini una vigezo vinavyotakiwa, usipoteze muda! Hii ni nafasi ya kipekee kujiunga na utumishi wa umma.
Kumbuka:
- Tuma maombi yako kwa usahihi kupitia mfumo rasmi wa Sekretarieti ya Ajira.
- Hakikisha unaambatanisha vyeti vyote muhimu.
- Soma tangazo kamili kwenye tovuti ya UTUMISHI kwa maelekezo ya kina.
Imeandikwa na: Wikihii.com
Tarehe: 12 Juni 2025
Chanzo: Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira