Tangazo la Nafasi za Kazi – Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu (Desemba 2025)
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu imetangaza nafasi tano (5) za ajira baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Waombaji wote wenye sifa wanahimizwa kuwasilisha maombi kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal.
Kwa nafasi nyingine zaidi zinazopatikana kila siku, tembelea Wikihii Jobs au ujiunge na WhatsApp Channel: Jobs Connect ZA.
1.0 Dereva Daraja la II – Nafasi 2
1.1 Majukumu ya Kazi
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi kwenye maeneo mbalimbali kwa shughuli za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari kwenye daftari (Log Book).
- Kufanya usafi wa gari.
- Kutekeleza majukumu mengine atakayoelekezwa na msimamizi wake.
1.2 Sifa za Mwombaji
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
- Leseni ya Daraja E au C, iliyotumika kwa angalau mwaka mmoja bila ajali.
- Cheti cha mafunzo ya udereva (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Vyeti vya ziada vya udereva vinavyotoa sifa ya kupata madaraja husika.
Ngazi ya mshahara
TGS B
1.3 Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 3
Majukumu ya Kazi
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni, kusikiliza changamoto zao na kuwaelekeza sehemu husika.
- Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, vikao, safari na ratiba za kazi.
- Kutafuta majalada/nyaraka zinazohitajika kutekeleza majukumu.
- Kupokea na kusambaza majalada kwa maofisa wa Divisheni/Kitengo husika.
- Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada sehemu zinazohusika.
- Kuandaa dondoo na maandalizi ya vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
Sifa za Mwombaji
- Kuwa na Elimu ya Form IV au Form VI.
- Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6).
- Kufaulu Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza (maneno 100 kwa dakika).
- Ujuzi wa kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher.
- Cheti kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya Mshahara
TGS C
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Waombaji wawe Raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 – 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na kuainisha ulemavu kwenye mfumo wa Ajira Portal.
- Ambatanisha C.V yenye maelezo kamili, namba za simu, email na majina ya referees watatu.
- Vyeti vya elimu na taaluma vithibitishwe na Mwanasheria/Wakili.
- Vyeti vya kitaaluma na vya Form IV/Form VI ni lazima viwe halisi; Result slips hazitakubaliwa.
- Vyeti vya nje ya nchi vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTVET.
- Wastaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kada ya Dereva II wawasilishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
- Waajiriwa wa nafasi za kuingia ndani ya utumishi wa umma hawapaswi kuomba.
- Waliogushi nyaraka watakumbana na hatua za kisheria.
- Majina yanayokinzana kwenye nyaraka yahakikiwe kwa Deed Poll.
Mwisho wa Kutuma Maombi
08 Desemba 2025
Anuani ya Kutuma Maombi (Barua)
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu,
S.L.P. 50,
Ushetu – Kahama.
Namna ya Kutuma Maombi
Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal kupitia kiungo:
Maombi nje ya mfumo wa Ajira Portal hayatafanyiwa kazi.
Hitimisho
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu imefungua milango kwa waombaji wenye sifa kuomba nafasi hizi za uhazili na udereva. Hakikisha unaandaa nyaraka sahihi, zilizothibitishwa, na unawasilisha maombi kabla ya tarehe ya mwisho.
Kwa nafasi zaidi za ajira serikalini na sekta binafsi, tembelea Wikihii.com au ujiunge na WhatsApp Channel yetu kwa updates: Jobs Connect ZA.
Limetolewa na:
Hadija M. Kabojela
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu

