Kwenye hii article tunaenda kukupa maelekezo ya siri za forex biashara ambayo imefichwa (inajulikana na wachache) kwa sababu ya sifa za kuwa na utajiri mkubwa endapo kama utaifahamu vzr hii biashara ya forex, basi kaa tayari kwa sababu safari ya mafunzo inaanza sasa, na tunaanza na ukweli kuihusu biashara ya forex trading
Forex tunayoizungumzia hapa tunaifanya kupitia platform maalum kama vile Metatrader4, Metatrader5 au Tradingview, na tunatumia madalali wa forex (brokers) maalum kununua na kuuza pesa za nchi mbalimbali (currency trading -forex).
Kwenye masoko ya forex bei zinapanda na kushuka mara kwa mara kitendo hichi kwenye trading tunakiita market volatility na kimsingi hapo ndipo forex trader anapoweza kutengeneza pesa akiwa na maarifa ya forex trading kwa sababu forex tunaifanya kwa kufanya mambo mawili tu kuuza na kununua (buy and sell), swali linakuja unauza wakati gani?, au unanunua wakati gani?, majibu yako unayapata kwenye paragraph inayofuata.
Soma Hii: BIASHARA YA FOREX PDF
Mpango mzima kwenye forex ni kwamba unanunua pale unapohisi bei itapanda – ikipanda kweli unapata faida wakati huohuo kama bei ikishuka unapata hasara, Lakini pia unauza pale unapohisi kwamba bei itashuka -ikishuka kweli unakuwa unapata faida na wakati huohuo ikiwa inapanda unakuwa unapata hasara.
Kinachotakiwa kwenye hii biashara ya forex ni kufanya predictions sawasawa, kwa sababu kitu pekee ambacho ni naamini ni kweli ni kwamba bei ikienda upande wako kama umenunua au umeuza basi unapata faida tena kadri bei inavyozidi kwenda upande wako wa mtaji wako unakuwa unaendelea kupanda direct kwenye metatrader platforms,
Kitu kimoja twende sawa ninaposema prediction au kuhisi kama bei itapanda au itashuka hii sio bahati nasibu, na wala sio betting, kwenye forex tunahisi bei itapanda au kushuka kwa kutumia mbinu zake maalum za kitaalamu na nyingine za kiuchumi zinazotambulika kufanya uchambuzi kwenye masoko ya forex.
Bofya kutumia Forex Tools
Tembelea pages zetu za Forex – kama Kalenda ya Uchumi, Viwango vya fedha, Pips Calculator, Position Size Calc, Lot Size Calc, Time Zone (Market Hours)
Fungua Forex ToolsMaana ya Forex pairs
Kwenye forex tunachotrade hasa ni pairs, mfano wa pair ni kama GBPUSD, EURUSD, XAUUSD, USDJPY na nyingine nyingi cha msingi hapa ni kwamba kuna MINOR PAIRS na MAJOR PAIRS, yaani pairs kubwa na ndogo,
Tuchukulie mfano wa GBPUSD PAIR – hii ni pair ambayo inajumuisha pesa za nchi mbili tofauti kuna GBP ambayo ni kifupi cha British Pound, halafu kuna USD ambayo ni kifupi cha United States Dollar, Pesa au currencies hizi mbili zinatrade against each other, yani GBP akiwa anapanda wakati huohuo USD anakuwa anashuka na Viceversa its true.
Kupanda au kushuka kwa bei katika soko lolote kunasababishwa na mambo mengi inaweza kuwa news, inaweza kuwa sera za benk kuu ktk nchi husika, inaweza kuwa hali ya vita au matukio mengine yanayoweza kuathiri masoko ya currencies (forex), Soko la forex linafanya kazi siku 5 za wiki hii ina maana masoko ya forex hayafanyi kazi weekend.
Session zilizopo kwenye forex
Kuna masoko mbalimbali ya kidunia ya forex hapa sasa nazungumzia market sessions, hapa tuna masoko makubwa manne duniani kote ambayo ni LONDON SESSION, NEWYORK SESSION, SYDNEY SESSION na TOKYO SESSION.
Hizo session hapo juu ndio ufunguo wako kwa sababu hizo session ndio zinakuonesha kwamba mabenk ya United Kingdom (UK) sasa yamefunguliwa ikiwa ni London session, au Mabenki ya USA sasa yamefunguliwa ikiwa ni NY session na kadhalika wakati huohuo kwenye trading tunatakiwa kufanya bishara wakati ambao traders wengi wapo live online kwa sababu tunahitaji Volume ya traders wakiwa wengi maana yake kutakua na nguvu kubwa ya kuweza kupush na kwenda uelekeo fulani (uptrend, Downtrend).
Soko la forex lipo huru mtu yeyote anaweza kufanya trading kinachotakiwa ni PC/Laptop yako na access ya internet everytime, lakini sasa ni wakati wa kuwajua wahusika wakubwa kwenye masoko ya forex hapa namaanisha watu au makampuni ambayo nayo yanaishi kwa kufanya forex trading kama ambavyon wewe unayesoma hii makala unatamani kuishi kwa kufanya forex Wahusika wakubwa ni Benki mbalimbali, Makampuni yanayofanya kazi ya ku manage mitaji mikubwa kitaalamu tunayaita HEDGE FUNDS MANAGEMENT COMPANIES, Forex Brokers wenyewe, Serikali yoyote ile itahusika kwenye forex kupitia sera mbalimbali za kiuchumi au kupitia benki kuu ambayo inajulikana kwa uwezo wake wa kushusha au kupandisha interest rate (riba) ambayo hupelekea volatility kubwa sana kwenye soko husika.
Bofya kutumia Forex Tools
Tembelea pages zetu za Forex – kama Kalenda ya Uchumi, Viwango vya fedha, Pips Calculator, Position Size Calc, Lot Size Calc, Time Zone (Market Hours)
Fungua Forex ToolsPlatform zinazotumika kwenye forex
Kwenye trading tunatumia platforms maalum kwa ajiri ya ku trade hapa namaanisha METATRADER4 (MT4) na METATRADER5 (MT5) Hizi ni platform maalum kwa ajiri ya kuingia na kutoka kwenye trade pamoja na kufanya trade management kuweka Stop Loss, Take profit na kadhalika, Lakini ili tufungue trade (position) tunatakiwa kuwa na account real kutoka kwa dalali wa forex (BROKER) hapa kuna machaguo mengi hawa forex brokers wapo wengi sana kwa mfano kuna TD365, FBS, XM, EXNESS List inaendelea kwa sababu wapo wengi sana cha kuzingatia hapa ni kwamba kila broker anatofautiana na mwingine interms of services offered, kwa hiyo ni vzr kusoma na kuelewa conditions a broker kama zitakufaa kabla ya kufungua account na broker huyo,
Itaendelea hivi karibuni