Utajiri wa Alikiba Mwaka 2025: Mfalme wa Bongo Fleva
Ali Saleh Kiba, maarufu kama Alikiba au “King Kiba”, ni msanii wa muziki wa Bongo Flava kutoka Tanzania ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na vipaji vyake vya kipekee katika uimbaji na uandishi wa nyimbo. Mbali na mafanikio yake katika muziki, Alikiba pia ameweza kujenga utajiri mkubwa kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato. Akiwa kama mkongwe kwenye kizazi kipya cha muziki Ali ametumia vzr fursa mbalimbali kuweza kujitengenezea pesa na mali anazomiliki.
Vyanzo vya mapato ktk Utajiri wa Alikiba
1. Mapato Kutoka kwenye Muziki
Alikiba alianza kujulikana mwaka 2004 baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza “Maria”, na baadaye akapata umaarufu mkubwa kupitia albamu yake ya “Cinderella” mwaka 2008. Nyimbo zake kama “Mwana”, “Aje”, na “Chekecha Cheketua” zimekuwa maarufu sana na kumletea mapato makubwa kupitia mauzo ya muziki na maonyesho ya moja kwa moja.
2. Mikataba ya Udhamini na Biashara za Alikiba
Mbali na muziki, Alikiba amekuwa akipata mapato kupitia mikataba ya udhamini na biashara mbalimbali. Amesaini mikataba na kampuni kubwa kama Sony Music Entertainment, ambapo alikuwa msanii wa pili barani Afrika kusaini mkataba na kampuni hiyo mwaka 2016. Ingawa aliachana na Sony mwaka 2021, mkataba huo ulimletea mapato na umaarufu wa kimataifa.

3. Mapato Kutoka YouTube channel ya Alikiba
Alikiba ana channel ya YouTube yenye zaidi ya subscribers milioni 2.07 na jumla ya views zaidi ya milioni 500. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2025, mapato yake ya kila mwezi kutoka YouTube yanakadiriwa kuwa kati ya $4,000 hadi $5,000, ambayo ni sawa na zaidi ya Tsh milioni 10 kwa mwezi.
4. Mali na Uwekezaji wa Alikiba
Alikiba pia amewekeza katika mali isiyohamishika na biashara nyingine. Anamiliki nyumba ya kifahari katika maeneo ya juu ya jiji la Dar es Salaam na magari ya kifahari kama Range Rover na Mercedes–Benz. Pia, ameanzisha lebo yake ya muziki, Kings Music Records, ambayo inasaidia kukuza vipaji vipya vya muziki nchini Tanzania. Bila kusahau sasa hivi amefungua kituo cha TV (CrownMedia) akiwa ameshirikiana na mkongwe wa habari Salim Kikeke.
5. Makadirio ya Utajiri wa Alikiba
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, utajiri wa Alikiba unakadiriwa kuwa kati ya $2.2 milioni hadi $4.5 milioni kwa mwaka 2025, ambayo ni sawa na zaidi ya Tsh bilioni 5. Hii inamuweka katika nafasi ya pili au ya tatu miongoni mwa wasanii matajiri zaidi nchini Tanzania, akifuatia Diamond Platnumz na Vanessa Mdee
6.Kituo cha Crown Media
Alikiba, msanii maarufu wa Bongo Flava, alizindua rasmi kampuni yake ya vyombo vya habari, Crown Media, mnamo Machi 9, 2024, katika hafla ya kifahari iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Crown Media inajumuisha kituo cha redio, Crown FM 92.1, kinachorusha matangazo katika maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, na Pwani, pamoja na kituo cha televisheni, Crown TV, kinachopatikana kupitia Azam TV.
Kwa mujibu wa Alikiba, alihamasishwa kuanzisha Crown Media kutokana na mapenzi yake ya muda mrefu kwa vyombo vya habari na athari chanya aliyopata kutoka kwa redio ndogo aliyozawadiwa na baba yake alipokuwa mdogo. Kupitia Crown Media, Alikiba analenga kutoa burudani ya kiwango cha juu, habari, na maudhui yanayoburudisha na kuelimisha jamii, huku akiwapa wasanii chipukizi jukwaa la kuonyesha vipaji vyao.
Je, unajua utajiri wa Diamond Platnumz?
Fahamu vyanzo vyake vya utajiri, biashara alizojenga, na mapato yake ya kifahari. Soma makala kamili na ujifunze zaidi kuhusu safari ya mafanikio ya msanii huyu maarufu!
Soma Makala KamiliMfalme wa Bongo Flava @OfficialAliKiba anatarajiwa kukabidhiwa tuzo ya heshima ya maisha kutoka @nxthonors siku ya leo. Tukio zima litaonyeshwa live kupitia chaneli ya Youtube ya TOP CHARTS.
— Crown Media (@CrownMediaTZ) January 31, 2025
King Kiba anakuwa msanii wa kwanza ambaye sio Mnigeria kushinda tuzo hiyo kutokana na… pic.twitter.com/aOyZbxe9cO