Utajiri wa Diamond Platnumz 2025: Simba wa Africa
Diamond Platnumz, ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul , si tu msanii wa Bongo Flava, bali ni mfano halisi wa mafanikio ya kijana wa Kiafrika aliyepambana kutoka chini hadi kileleni. Kutoka kuishi katika chumba kimoja na mama yake huko Tandale, hadi kuwa mmoja wa wasanii matajiri zaidi Afrika — lifestory ya Diamond ni ya kuvutia na yenye mafunzo mengi sana huwezi kuamini kwamba Diamond wa leo ni mfanyabiashara mkubwa sana Tanzanaia na hivi karibuni amezindua biashara mpya ya Wasafi Soap.
Mapato ya Muziki
Diamond Platnumz alianza kuvuma mwaka 2010 kupitia wimbo “Kamwambie”, na tangu hapo ametoa nyimbo nyingi zilizoshika chati ndani na nje ya Afrika kama Number One, Jeje, Waah!, Inama na Yatapita.
Kulingana na taarifa mbalimbali, Diamond hupata zaidi ya USD 30,000 hadi 60,000 kwa show moja ya kimataifa na kati ya TSh 30 milioni hadi 50 milioni kwa show ya ndani.
YouTube Monetization na Mapato ya Kidijitali
Diamond Platnumz ni msanii wa kwanza Afrika Mashariki kuvuka subscribers milioni moja kwenye YouTube, na sasa ana zaidi ya subscribers milioni 8 na views zaidi ya bilioni 2.5.
Kulingana na makadirio ya wastani, Diamond hupata kati ya USD 5,000 hadi 10,000 kwa mwezi kupitia mapato ya YouTube pekee — ambayo ni zaidi ya TSh milioni 20 kwa mwezi.
Wasafi Media: Redio na Televisheni
Mwaka 2018, Diamond alizindua kampuni ya Wasafi Media inayoendesha Wasafi FM na Wasafi TV. Hizi zimekuwa chombo kikubwa cha kuendesha biashara na kueneza kazi zake.
Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti za ndani, Wasafi Media hupokea zaidi ya TSh milioni 100 kwa mwezi kutoka kwa wadhamini na matangazo ya biashara.
WCB Wasafi: Lebo ya Muziki
Diamond pia ni mwanzilishi wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi ambayo imewasign wasanii wakubwa kama Diamond platnumz, Zuchu, Lavalava, D Voice na wengine. Wasafi ni Lebo kubwa sana africa na imehusika kuwatoa kwenye mainstream wasanii wengi ambao sasa ni wakubwa na wanajitegemea kama Harmonize na Rayvanny Lebo hii hupata mapato kupitia usimamizi wa kazi za wasanii, bookings, na mauzo ya kidijitali.
Kwa mfano:
- Zuchu alifikisha streams milioni 100 ndani ya mwaka mmoja — mapato haya yote yanapita pia kwenye mifumo ya WCB Management.
- Rayvanny alipokuwa chini ya WCB Management, alifanya show zaidi ya 40 kwa mwaka, na mapato hayo yalichangia utajiri wa lebo.
Maisha Binafsi, Majumba na Magari ya Diamond
Diamond anaishi katika nyumba ya kifahari ya serena white mansion iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam, ambayo inasemekana ilimgharimu zaidi ya TSh bilioni 1. Pia amenunua jumba Dubai ambalo alisema limegharimu zaidi ya USD 1.5 milioni.
Magari anayomiliki Diamond ni pamoja na:
- Rolls Royce Cullinan – gari la kifahari lenye thamani ya zaidi ya TSh 1.3 bilioni
- Cadillac Escalade
- BMW X6, Toyota Land Cruiser V8, Toyota Alphard na magari mengine ya kifahari
Diamond Platnumz ni balozi wa Makampuni Makubwa
Diamond amekuwa balozi wa bidhaa na makampuni mbalimbali kama:
- Pepsi
- Parimatch
- Coral Paints
- NMB Bank
Makubaliano ya ubalozi wa makampuni haya huleta mapato ya mamilioni ya shilingi kwa mwaka. Kwa mfano, dili na Coral Paints inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya TSh milioni 500.
Biashara za Diamond Platnumz Nje ya Muziki
Mbali na muziki, Diamond pia ni mfanyabiashara:
- Ameanzisha bidhaa ya Sabuni ya “Wasafi Soap”.
- Anamiliki duka la nguo “Wasafi Collection”.
- Amewekeza kwenye Betting “WasafiBet”.
- Amewekeza kwenye Kituo cha Redio & TV “Wasafi Media”.
Makadirio ya Utajiri Wa Diamond Platnumz
Kulingana na vyanzo vya ndani na uchambuzi wa mapato yake, utajiri wa Diamond Platnumz unakadiriwa kuwa zaidi ya USD 10 milioni (zaidi ya TSh bilioni 25), na baadhi ya wachambuzi wanadai anaweza kuwa na zaidi ya USD 20 milioni ukihesabu mali zisizohamishika na biashara anazomiliki.
Diamond Platnumz: Mfano wa Kuigwa Afrika
Diamond Platnumz si msanii tu bali ni chapa ya biashara, balozi wa kizazi kipya cha vijana wa Kiafrika wenye ndoto kubwa. Safari yake inathibitisha kuwa muziki unaweza kuwa si burudani tu bali chanzo kikubwa cha utajiri na mabadiliko chanya ya jamii.
Utajiri wa diamond forbes
Utajiri wa Diamond Platnumz Kulingana na Forbes, Diamond Platnumz, msanii wa Bongo Flava kutoka Tanzania, amekuwa mmoja wa wanamuziki matajiri zaidi barani Afrika. Kwa mujibu wa makadirio mbalimbali, ikiwemo maoni kutoka kwa jarida la Forbes Afrika, utajiri wake unakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 7 za dola za Kimarekani (zaidi ya Tsh bilioni 17).Hii ni kutokana na mafanikio yake ya kimuziki, mikataba ya ubalozi wa bidhaa, mapato kutoka YouTube, pamoja na biashara binafsi alizozianzisha. Umaarufu wake umevuka mipaka ya Afrika Mashariki, na kumletea fursa za kiuchumi ambazo wasanii wengi wa kizazi chake hawajazifikia.Mbali na muziki, Diamond ana miradi kadhaa mikubwa ya kibiashara kama vile WCB Wasafi (label ya muziki), Wasafi Media (radio na TV), Wasafi Bet, Wasafi Collection. Akiwa pia balozi wa makampuni makubwa kama Pepsi na NMB Bank, Diamond ameweka jina lake kuwa nembo ya kibiashara.Ingawa Forbes haijamuweka rasmi kwenye orodha ya matajiri 10 bora wa Afrika, amewahi kuorodheshwa kama miongoni mwa wasanii wanaopata pesa nyingi kupitia muziki na mitandao, akizidiwa na mastaa kama Akon na Burna Boy tu kwa upande wa Afrika.
Diamond Platnumz alishiriki katika mfululizo maarufu wa Netflix uitwao “Young, Famous & African”, ambao ulianza kurushwa mwaka 2022. Series hii inaangazia maisha ya mastaa wa Kiafrika maarufu na matajiri kutoka nchi mbalimbali, wakiishi Johannesburg, Afrika Kusini. Diamond alionekana katika misimu ya kwanza na ya pili, na alirejea tena katika msimu wa tatu ulioanza Januari 2025 Ingawa ushiriki wake katika “Young, Famous & African” umeongeza umaarufu wake na kumsaidia kufikia hadhira pana zaidi, bado haijulikani wazi ni kiasi gani cha mapato anayopata moja kwa moja kutoka kwa series hii.!
Fahamu Siri ya Mafanikio ya Chief Godlove!
Unataka kujua jinsi kijana huyu Mtanzania alivyojijengea jina kama mmoja wa matajiri wanaochipukia? Soma makala yetu kamili kuhusu safari yake ya mafanikio, biashara alizonazo, na vyanzo vyake vya mapato.
Soma Makala KamiliMaswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Utajiri wa Diamond Platnumz
1. Diamond Platnumz ana utajiri wa kiasi gani?
Kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni, Diamond Platnumz anamiliki utajiri unaokadiriwa kuwa zaidi ya dola milioni 7 za Kimarekani (zaidi ya Tsh bilioni 17). Chanzo chake kikuu cha mapato ni muziki, biashara binafsi, na mikataba ya kibiashara.
2.Diamond Platnumz Ana biashara gani kubwa zinazomletea mapato?
Diamond anamiliki biashara mbalimbali ikiwemo WCB Wasafi (label ya muziki), Wasafi Media (TV na redio), Wasafi Bet (michezo ya kubashiri), Wasafi Collection (mavazi), na Chibu Perfume (manukato).
3. Je, Diamond huingiza pesa kiasi gani kupitia YouTube?
Channel ya YouTube ya Diamond Platnumz imevuka subscribers milioni 8, na inakadiriwa kuingiza zaidi ya dola 30,000 kwa mwezi kupitia matangazo pekee.
4.Diamond Platnumz Ana nyumba au mali za kifahari?
Ndiyo. Diamond anamiliki nyumba ya kifahari Mbezi Beach – Dar es Salaam, nyumba nyingine Johannesburg (Afrika Kusini), na pia alithibitisha kuwa na nyumba Dubai. Pia ana magari ya kifahari kama Rolls Royce, Cadillac, na Land Cruiser.
5. Je, Forbes imemuweka Diamond Platnumz kwenye orodha ya matajiri Afrika?
Ingawa Forbes Afrika haijamtaja rasmi kwenye orodha ya “Top 10 Richest Africans”, wamemtambua kama mmoja wa wasanii wa Afrika waliopiga hatua kubwa kibiashara.
6.Diamond Platnumz Ana vyanzo gani vya kipato?
Mbali na muziki, Diamond hupata kipato kupitia mikataba ya ubalozi wa bidhaa (kama Pepsi na NMB), matamasha ya kimataifa, na mapato kutoka kwa streaming platforms kama Boomplay, Spotify, na Apple Music.