Nafasi za Kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ)
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa kushirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linakaribisha maombi kutoka kwa vijana wa Kitanzania waliotayari kulitumikia taifa kupitia jeshi kwa mwaka 2025.
Huu ni mwaliko rasmi kwa vijana wote waliokidhi vigezo, kuwasilisha maombi yao kufuata utaratibu uliowekwa na Makao Makuu ya TPDF.
Maelekezo ya Jumla kwa Waombaji:
Waombaji wote wanatakiwa kuandika barua rasmi ya maombi, ikieleza dhamira ya kujiunga na JWTZ.
Nyaraka za Kuambatisha:
- Cheti cha kuzaliwa
- Vyeti vya elimu (Kidato cha Nne/Kidato cha Sita/Vyuo)
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Picha ndogo (passport size)
NB: Waombaji wote watajulishwa tarehe ya usaili baada ya uchambuzi wa awali wa nyaraka.
Sifa za Kujiunga na JWTZ:
- Awe Raia wa Tanzania
- Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha Nne na awe amefaulu
- Awe hajaoa wala hajaolewa
- Umri uwe kati ya miaka 18 hadi 25
- Awe na tabia njema na mwenendo mzuri
- Awe na afya njema ya mwili na akili
Nafasi za Maafisa (Officer Cadet):
Kwa wale waliomaliza Kidato cha Sita na kuendelea, wanaweza kuwania nafasi za mafunzo ya Uafisa.
- Uchaguzi hufanywa na Officers Selection Board
- Watakaochaguliwa watapewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet)
- Mafunzo yatafanyika katika Tanzania Military Academy (TMA) kwa kipindi cha mwaka mmoja
Anuani ya Kutuma Maombi:
Tanzania People’s Defense Force (TPDF)
P.O. Box 194
Miyubi / Msalato
Dodoma – Tanzania
Chini ni sample barua ya kuomba Nafasi za Kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ)
Maswali yanayoulizwa sana kuhusu Nafasi za Kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) /FAQs
Ninaweza kuomba ikiwa nimeoa/nimeolewa?
Hapana. Moja ya vigezo muhimu ni kuwa hujaoa wala kuolewa wakati wa kuomba nafasi hizi
Je, umri ukizidi miaka 25 na bado niko katika hali nzuri kiafya, naweza kuomba?
Samahani, umri wa mwisho ni miaka 25 kwa waombaji wapya. Ikiwa umevuka umri huo, huwezi kuendelea na maombi haya.
Vyeti vya awali vinatakiwa kuwa na alama fulani?
Ndiyo, unatakiwa uwe umefaulu angalau kwa kiwango kinachokubalika na wizara ya elimu. Hii ni pamoja na ufaulu wa masomo ya msingi ya sekondari.
Maombi yanatumwa kwa njia ya mtandao au kwa posta?
Kwa sasa, maombi yanatumwa kwa njia ya barua ya kawaida kupitia anuani ya posta iliyoainishwa:
TPDF, P.O. Box 194, Miyubi / Msalato, Dodoma – Tanzania
Nitatumiwa lini taarifa ya usaili?
Baada ya uchambuzi wa awali wa nyaraka zako, utapokea taarifa rasmi ya tarehe na sehemu ya usaili kupitia njia utakayoainisha kwenye barua yako (anwani au simu).
Je, wanawake wanaruhusiwa kuomba?
Ndiyo. Vijana wa kike na wa kiume wote wanaruhusiwa kuomba, alimradi watimize vigezo vyote vilivyowekwa.
Mafunzo ya maafisa (Officer Cadet) yanafanyika wapi?
Mafunzo haya hufanyika katika Chuo cha Kijeshi cha Tanzania (Tanzania Military Academy – TMA) kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Download maswali yanayoulizwa sana kuhusu Nafasi za Kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ)